Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 27.12.2017

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsenal Mesut

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 29, yuko namba moja katika orodha ya Barcelona lakini mabingwa hao wa La Liga wanataka kuwasaini wachezaji watano mwezi Junuari. (Marca via Daily Express)

Southampton hatimaye wamekiri kushindwa kumweka beki Virgin Van Dijk, 26, lakini hawatamuuza chini ya pauni milioni 70. (Sun)

Meneja wa Everton Sam Allardyce aamini kuwa mshambuliji wa Arsenal's Olivier Giroud atahamia Goodison Park mwezi Junuari.(Liverpool Echo)

Arsenal wako tayari kumpa mkataba wa muda mrefu kiungo wao wa kati Jack Wilshere 25. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Emre Can

Juventus watamtumia wing'a Marko Pjaca,22, kama sehemu ya makubaliano kumsaini kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can, 23. (Tuttosport, kupitia ESPN)

Jose Mourinho anataka kuengeza namba ya 10 katika kikosi chake cha Manchester United mwezi January. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi bado hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo huku Real Mdrid wakimmezea mate nchezaji huyo wa miaka 24. (Calciomercato, kupitia Daily Express)

West Ham wanammezea mate kiungowa kati wa Sevilla Steven N'Zonzi, 29, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Arsenal na Everton. (Sun)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marouane Fellaini

Marouane Fellaini, 30, hana uhakika ikiwa atasalia Manchester United hata kama mkataba wake utaboreshwa. (Humo kupitia Manchester Evening News)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amakataa kukana ofa ya pauni milioni 53 kumnunua kiunga wa kati wa Bayern Munich Arturo Vidal, 30. (Daily Mail)

Mada zinazohusiana