Conte asema Chelsea haina bahati msimu huu

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte ametaja ukosefu wa bahati katika kikosi chake kama sababu ya wao kuwa pointi 13 nyuma ya viongozi wa ligi Manchester City
Image caption Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte ametaja ukosefu wa bahati katika kikosi chake kama sababu ya wao kuwa pointi 13 nyuma ya viongozi wa ligi Manchester City

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte ametaja ukosefu wa bahati katika kikosi chake kama sababu ya wao kuwa pointi 13 nyuma ya viongozi wa ligi Manchester City baada ya ushindi mzuri dhidi ya klabu ya Brighton.

Kikosi hicho cha Conte kilirekodi ushindi wa sita mfululizo nyumbani baada ya kuonyesha mchezo mzuri ulioimarika katika kipindi cha pili dhidi ya Seagulls huku Alvaro Morata na Marcos Alonzo wakifunga mabao muhimu.

Lakini mabingwa hao wa ligi ya Uingereza wanasalia katika nafasi ya tatu huku City wakijiandaa kukabiliana na Newcastle siku ya Jumatano.

''Msimu huu uko tofauti na msimu uliopita'', alisema Conte baada ya mechi hyo iliochezwa siku ya siku kuu ya Boxing Day.

''Msimu uliopita mara nyingi tulishinda mechi na tulikuwa na bahati, kama vile dhidi ya West Brom hapa na Sunderland. Msimu huu mara nyengine tungekuwa na bahati zaidi''.

''Tunaiheshimu sana Manchester City kwa sababu wanafanya kitu kisichokuwa cha kawaida''.

Image caption Antonio Conte

Kikosi cha Conte hakikuwa na bahati katika kipindi cha kwanza ambapo mfumo wa kocha Chris Hugton wa 4-5-1 uliwazuia Chelsea licha ya timu hiyo kushambulia kupitia Tiemoue Bakayoko na Victor Moses.

Lakini Brighton walipatikana wamezubaa kunako sekundi ya 52 ya kipindi cha pili wakati Morata alipowachenga mabeki na kufunga krosi ya Cesar Azpilicueta's kupitia kichwa.

Bao hilo lilibadilisha mambo na kuimarisha shinikizo ya timu hiyo ya nyumbani ambayo ilimtumia Eden Hazard katika jaribio la kuvunja ulinzi uliowekwa na wageni hao.

Lakini ilikuwa Alonzo aliyefunga udhia kupitia kichwa muda mfupi baada ya kukosa mabao mawili kutokana na mpira wa adhabu na kichwa.

''Katika kipindi cha pili ,tuliimarika na kutengeza nafasi nyingi'', aliongezea Conte.

''Ulikuwa mchezo mzuri''.

Mada zinazohusiana