Virgil van Dijk kujiunga na liverpool kwa pauni milioni 75

Beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk

Beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk atajiunga na Liverpool wakati wa dirisha la uhamisho tarehe moja mwezi Januari kwa mkataba wa rekodi ya kimataifa ya £75m.

Raia huyo kutoka Uholanzi alitarajiwa kujiunga na Reds msimu uliopita baada ya kuomba uhamisho kutoka kwa klabu yake.

Lakini uhamisho huo haukufaulu pale Liverpool ilipoomba msamaha kwa madai ya kumtafuta mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kinyume cha sheria.

Arsenal yatoka sare ya 3-3 na Liverpool EPL

Mshambuliaji wa Southampton Charlie Austin apigwa marufuku ya mechi tatu

Ada hiyo ni kubwa ambayo hakuna beki yoyote awewahi kupokea - Manchester City iliipa Monaco £52m kwa Mbeligiji Benjamin Mendy mwezi Julai.

Van Dijk amesema kwenye taarifa yake , ''amefurahia'' kusaini kwa mkataba na klabu ya Merseyside na amekiri amekuwa na wakati mgumu '' kwa miezi michache iliyopita'' akiwa Southapton.

Beki huyo aliwachwa nje ya mchezo kwenye mechi ya Premia waliposhindwa magoli 5-2 na Tottenham siku ya Jumanne, hali iliyo

Mada zinazohusiana