Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 28.12.2017

Mshambuliaji wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 26 Antoine Griezmann. (Marca)
Image caption Mshambuliaji wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 26 Antoine Griezmann. (Marca)

Manchester United haitashindana na Barcelona katika kutaka kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 26 Antoine Griezmann. (Marca)

Paris St-Germain wanachunguza hali ya Marouane Fellaini katika uwanja wa Old Trafford na wako tayari kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 katika uhamisho wa bure msimu ujao.(Daily Mirror)

Liverpool ilimsafirisha daktari wake ili kuchunguza hali ya kimatibabu ya beki wa Southampton , 26, Virgil van Dijk ili kuweza kukamilisha usajili wa dau la £75m haraka iwezekanavyo - kabla ya Mancity kuwa na hamu ya mchezaji huyo.(Liverpool Echo)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Yannick Carrasco, 24, katika dirisha ka uhamisho la mwezi Januari(AS)

Atletico Madrid wanafurahia kumuuza winga Yannick Carrasco, 24, katika dirisha ka uhamisho la mwezi Januari(AS)

Chelsea ilifeli katika harakati za kutaka kumsajili mchezaji huyo wa Ubelgiji msimu uliopita lakini inaweza kuwasilisha ombi jingine. (Sun)

West Ham United inakaribia kumsajili beki wa Swansea mwenye umri wa miaka 23 Alfie Mawson. (ESPN)

Image caption Medhi Benatia ,30,

Ombi la Arsenal la kutaka kumsajili beki Medhi Benatia ,30, kwa dau la £35m limekataliwa na Juventus

Everton inalenga kumsajili mshambuliaji wa Besiktas Cenk Tosun, 26, mwezi Januari na inaweza kulipa £20m kumnunua mchezaji huyo wa timu ya taifa la Uturuki. (Liverpool Echo)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Abdoulaye Doucoure, 25,

Watford wameanza mazungumzo na kiungo wa kati Abdoulaye Doucoure, 25, kuhusu mkataba mpya wa miaka mitano ambao unaweza kuwa na thamani ya £70,000 kwa wiki. (Sun)

Mkufunzi wa zamani wa Sheffield Wednesday Carlos Carvalhal anatathminiwa kuchukua ukufunzi wa klabu ya Swansea. (Sun)

Image caption Jack Wilsheer

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kwamba kiungo wa kati Jack Wilshere ,25, atatia saini kandarasi mpya iwapo atakubaliana kifedha (Sky Sports)

Birmingham ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Nigeria mwenye umri wa miaka ,24, Shehu Abdullahi kutoka klabu ya Cypriot Anorthosis Famagusta. (Birmingham Mail)

Crystal Palace, Everton na Burnley zina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Cameroon mwenye umri wa miaka 24 Karl Toko Ekambi. (France Football - in French)

Image caption Kepa Arrizabalaga, 23,

Athletic Bilbao wanasubiri majibu kutoka kwa kipa wao Kepa Arrizabalaga, 23, kuhusiana na mazungumzo ya kusaini kandarasi mpya na klabu hiyo licha ya hamu kutoka Real Madrid.(El Pais - in Spanish)

Norwich iko tayari kumsajili kiungo wa kati na mshambuliaji wa Lyon ,21, Aldo Kalulu, ambaye amekuwa katika mkopo katika klabu ya Sochaux. (France Football - in French)

Mshambuliaji wa Newcastle mwenye umri wa miaka 23 Aleksandar Mitrovic anataka kuondoka katika klabu hiyo. (Daily Mirror)

Image caption Mkufunzi wa zamani wa timu ya Uingereza Fabio Capello anasema kuwa ataondoka katika klabu ya ligi ya Uchina Jiangsu Suning mwaka ujao. (goal)

Mkufunzi wa zamani wa timu ya Uingereza Fabio Capello anasema kuwa ataondoka katika klabu ya ligi ya Uchina Jiangsu Suning mwaka ujao. (goal)

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA lina imani kwamba Uingereza itakuwa miongoni mwa mataifa yatakayopigiwa upatu kuandaa kombe la dunia la mwaka 2030. (Sun)

Mshambuliaji wa Uruguay Sebastian Abreu, 41, ameweka rekodi mpya ya dunia kwa kujiunga na klabu ya 26 tangu aanze kucheza soka. (Daily Mail)

Mkufunzi wa West Ham David Moyes amesema kuwa hatua ya kumsaidia mshambuliaji Marko Arnautovic kujiimarisha ilikuwa sawa na kumwambia kwamba hatocheza iwapo hataki kukimbia (Evening Standard)

Mada zinazohusiana