Swansea yamuajiri Carlos Carvalhal kuwa mkufunzi wake

Swansea City wamemteua aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Sheffield Wednesday Carlos Carvalhal kuwa mkufunzi mpya. Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Swansea City wamemteua aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Sheffield Wednesday Carlos Carvalhal kuwa mkufunzi mpya.

Swansea City wamemteua aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Sheffield Wednesday Carlos Carvalhal kuwa mkufunzi mpya.

Kocha mchezaji Leon Britton alikuwa akisimamia Swansea kwa muda tangu klabu hiyo iliopo chini ya jedwali la ligi imfute kazi Paul Clement mnamo tarehe 20 Disemba.

Carvalhal, 52, alifutwa kazi na klabu ya Wednesday mkesha wa siku ya krisimasi huku klabu hiyo ya daraja la kwanza ikiwa katika nafasi ya 15 katika jedwali la daraja la kwanza.

Raia huyo wa Ureno anajiunga na Swansea hadi mwisho wa msimu akiwa na fursa ya kuongeza mkataba huo.

Carvalhal ambaye ni mkufunzi wa tano wa Swansea katika kipindi cha miaka miwili, aliongoza Wednesday kufika katika raundi ya muondoano katika misimu miwili ilopita.

Mkufunzi huyo wa zamani wa klabu ya Besikitas , Sporting Lisbon na Maritimo ambaye alirithi mahala pake Stuart Gray huko Hillsborough mwezi Juni 2015 alifanikiwa kupata ushindi wa asilimia 42.7 katika mechi zake 131 alizosimamia.

Mada zinazohusiana