Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 30.12.2007

Cristiano Ronaldo
Image caption Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo ameitaka klabu ya Real Madrid kuweka bei yao ya kumuuza isiopungua £89m). Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kutoka Ureno yuko tayari kuondoka Uhispania.(Daily Record)

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, hajakaataa kuongeza kandarasi na mabingwa hao watetezi wa Uingereza licha ya madai kutoka kwa babake kwamba anataka kuhamia Real Madrid.(Independent)

Image caption Eden Hazard

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anajiandaa kumnunua winga wa Ivory Coast na Crystal Palace Zaha ili kuchukua mahala pake mshambulijai wa Chile Alexis Sanchez, 29. (Daily Star)

Wachezaji kadhaa wa Arsenal walidaiwa kumshutumu mshambuliaji Alexi Sanchez kwa kuwa na tabia mbaya baada ya mechi dhidi ya Burnley mwezi Novemba. (Guardian)

Image caption Winfred Zaha

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kuwa usajili wa kitita cha £75m wa beki wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 26 Virgil van Dijk kutoka Southampton haumanishi kwamba klabu hiyo sasa itamuuza Philippe Coutinho, lakini hakusema kuwa mchezaji huyo hataondoka Liverpool. (Daily Mail)

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anajiandaa kumnunua kiungo wa kati wa Everton na Uingereza Ross Barkley, 24. (Telegraph)

Image caption Ross Barkley

Manchester United inamchunguza kiungo wa kati wa Napoli na Itali Jorginho, 26, ili kuchukua mahala pake Michael Carrick. (Manchester Evening News)

West Ham itawasilisha ombi la kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Jonjo Shelvey, 25, huku David Moyes akijaribu kuimarisha safu yake ya kati.. (Daily Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Otamendi

Manchester City itampatia beki Nicolas Otamendi kandarasi mpya.Mchezaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 29 alitia kandarasi ya miaka 5 mwaka 2015(ESPN)

Nahodha wa West Brom Jonny Evans analengwa na klabu ya ManCity.

Mkufunzi wa klabu hiyo Alan Pardew alikiri kwamba klabu hiyo ingependelea kumuuza beki wa Ireland kaskazini Evans ili kukusanya fedha za kununua mshambuliaji (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Henrikh Mkhitaryan, 28.

Inter Milan inajiandaa kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Armenia Henrikh Mkhitaryan, 28. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge anapendelea uhamisho wa Southampton lakini anahofia United itazuia uhamisho wowote chini ya £25m. (Daily Mirror)

Hatahivyo Southampton inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Stoke ambayo inajiandaa kuongeza kiungo wa kati mwengine katika kikosi chake. (Mail)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Daniel Sturridge

Liverpool itamsajili kiungo wa kati wa Schalke's na Ujerumani Leon Goretzka katika uhamisho wa bure msimu ujao(Sun via Bild)

Juventus iko tayari kuanzisha makubaliano ya kuweka kandarasi na kiungo wa kati wa Liverpool na Ujerumani Emre Can, 23. (Corriere dello Sport - in Italian)

Mkurugenzi wa Everton Steve Walsh amesafiri hadi mjini Istanbul Uturuki ili kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Besiktas Cenk Tosun, 26, kufuatia waiwasi kutoka kwa vilabu vyengine vya Uturuki vinavyomuwinda (Times - subscription required)

Mada zinazohusiana