Mourinho ashangazwa na Klopp kununua mchezaji kwa dau la £75m

Mourinho ashangazwa na Klopp kununua mchezaji kwa dau la £75m
Image caption Mourinho ashangazwa na Klopp kununua mchezaji kwa dau la £75m

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amehoji madai ya mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp's ya mwaka 2016 kwamba yuko tayari kuwacha kazi yake badala ya kutumia fedha nyingi kununua wachezaji.

Liverpool inajianda kumsajili Virgil van Dijk kutoka Southampton kwa kitita cha £75m mnamo mwezi Januari, kitita ambacho kimevunja rekodi ya dunia kwa upande hamisho wa beki.

Klopp alisema siku ya Ijumaa kwamba kitu cha mwisho anachofikiria sio gharama kwa sababu wanampenda mchezaji huyo.

Aliongezea: Unapatiwa bei na ni lazima ukubali.

Hatahivyo Mourinho alitumia mkutano wake na wanahabri kuzungumzia kuhusu matamshi ya Klopp aliyotoa wakati United ilipomnunua Pogba kwa dau la £89m kutoka Juventus mnamo mwezi July 2016.

Klopp alinukuliwa akisema kwamba hawezi kununua mchezaji ni kiwango cha juu cha fedha na iwapo soka inaelekea katika mwelekeo huo basi huenda akawacha ukufunzi.

Mada zinazohusiana