Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 31.12.2017

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David Luiz

Barcelona watatoa ofa ya pauni milioni 130 kumnunua Coutinho, 25, wiki hii, na wana uhakika kuwa watampata mchezaji huyo wa Liverpool ambaye walikosa kumnunua msimu uliopita. (Sunday Mirror)

Arsenal wana nia ya kumsaini beki wa Chelsea David Luiz, lakini ikiwa Chelsea hawataki kuumuuza mchezaji huyo wa miaka 30 kwa mahasimu wao basi mbrazil huyo ataelekea Juventus. (Sunday Express)

West Ham, wana mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea Andre Schurrle, 27, kutoka Borussia Dortmund. (Bild huko German)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Emre Can

Bayern Munich na Manchester City wanaaminiwa kujiunga katika mbio za kumpata kiungo wa kati wa Liverpol na Ujerumani Emre Can, 23. (Tuttosport - in Italian)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anasema hajui mipango ya mshambuliaji Alexis Sanchez kuhusu hatma yake katika klabu hiyo. (Sunday Times)

Ajenti wa Alexis Sanchez amezungumza na Manchester City kuwashawishi kumpa ofa ya mweze Januari mchezaji huyo ambaye anataka kuondoka Arsenal. (Metro)

Haki miliki ya picha Empics
Image caption Alexis Sanchez

Beki wa Manchester City Nicolas Otamendi, 29, anatarajiwa kupewa mkataba mpya na klabu hiyo. (ESPN)

Arsenal wabeibuka kuwa katika kumsaini Steven N'Zonzi, 29, kutoka Sevilla huku meneja wa Everton Sam Allardyce akikiri kuwa na mpango wa kuboresha safu yake ya mashambulizi na ulinzi. (Daily Star Sunday)

Everton, Southampton, Crystal Palace na West Ham wamehushwa na kumsaini mwezi Januari mshabuliaji wa Atletico Madrid Nicolas Gaitan 29. (AS)

Mada zinazohusiana