Ashley Young ashtakiwa kwa utovu wa nidhamu

Ashley Young has made 17 Premier League appearances for Manchester United this season Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ashley Young ashtakiwa kwa udhofu wa nidhamu

Mchezaji wa Manchester United Ashley Young ameshtakiwa kwa kukosa nidhamu na shirikisho la kandanda la FA.

Young, 32, alionekana kumgonga kwa mkono mshambuliaji wa Southampton, Dusan Tadic wakati wa mechi iliyotoka sare ya sufuri siku ya Jumamosi.

Refa Craig Pawson hakukiona kisa hicho na Young alistahili kujibu mashtaka hayo hadi leo Jumapili.

Young ambaye alijiunga na Manchseter United mwezi Juni mwaka 2011, alirudi katika kikosi cha England mwezi uliopita baada ya kutokuwepo kwa miaka minne unusu.

United wameshuka hadi nafasi ya tatu katika ligi ya Primia baada ya sare mara tatu mfululizo na kushindwa na Bristol City katika kombe la EFL.