Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 01.01.2018

Eden Hazard Haki miliki ya picha PA
Image caption Eden Hazard

Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 120 kwa mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, 26. (Sun)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekana kuwepo tofauti kati ya mshambuliaji Alexis Sanchez, 29, na wachezaji wengine. (Sky Sports)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, amekataa kukana kuwepo jitihada mpya kwa Sanchez baada ya Gabriel Jesus kupata jeraha wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumapili. (Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Theo Walcott

Southampton wanataka kumsaini wing'a wa Arsenal Theo Walcott 28, kwa mkono Januari hii. (Mail)

Na Arsenal wanaweza kumuchia mchezaji huyo kuondoka huku Everton, Watford na West Ham wakiwa na dalili za kumsaini. (Mirror)

Manchester United wanatumai kuwa kiungo wa kati Paul Pogba anaweza kumsaini mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, 24, kujiunga na klabu hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Joao Mario

Naye meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka kiungo wa kati wa Inter Milan Joao Mario 24, kuchukua mahala pake Michael Carrick, 36. (Sun)

Tottenham hawako mbioni kuafikia mkataba mpya na mlinzi Toby Alderweireld, 28, licha ya mkataka wake wa sasa kumruhusu kuondoka msimu wa joto wa mwaka 2019 kwa pauni milioni 25. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Schalke Leon Goretzka, 22, atajiunga na Bayern Munich msimu huu. (Bild - in German)

Mada zinazohusiana