Nani mbabe England: Mambo muhimu kuhusu Ligi ya Premia 2017

Manchester City and Chelsea Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Chelsea na Manchester City zimekuwa ndizo klabu zilizofana zaidi Ligi ya Premia mwaka 2017

Chelsea walishinda Ligi Kuu England msimu uliopita nao Manchester City wameanza kwa kishindo na kupanua mwanya wa alama 14 kileleni kufikia sasa.

Lakini kwa jumla 2017, nani alikuwa bora zaidi?

Harry Kane ni mchezaji aliyeng'aa sana, lakini alizishinda klabu ngapi, na mameneja kufutwa kulisaidia chochote?

Hizi hapa ni takwimu za kufafanua hayo, pamoja na matukio mengine mengi yaliyovunja rekodi 2017.

Nani anaongoza jedwali ukiangalia mwaka 2017?

Chelsea walishinda ligi msimu uliopita kwa kushinda mechi 30 kati ya 38 na kumaliza alama saba mbele ya Tottenham.

Msimu huu walizembea mwanzoni, na Manchester City ndio wamewika.

City wameshinda mechi 19 kati ya 21 kufikia sasa msimu wa 2017-18.

Ukiongeza mechi 11 walizoshinda nusu ya mwisho ya msimu uliopita, ndio bado wanaongoza 2017.

Msimamo wa jedwali EPL 2017
Nafasi Klabu Mechi Kushinda Sare Kushinda Mabao waliyofunga Mabao waliyofungwa Tufauti ya mabao Alama
1 Man City 40 30 8 2 102 30 +72 98
2 Chelsea 40 28 5 7 82 34 +48 89
3 Tottenham 40 27 6 7 92 33 +59 87
4 Man Utd 40 21 14 5 68 26 +42 77
5 Arsenal 41 23 7 11 76 51 +25 76
6 Liverpool 40 20 14 6 80 45 +35 74
7 Everton 40 17 10 13 62 53 +9 61
8 Burnley 40 13 12 15 36 43 -7 51
9 Leicester 40 14 9 17 55 64 -9 51
10 Swansea 40 13 6 21 37 58 -21 45
11 Crystal Palace 41 12 8 21 39 62 -23 44
12 Watford 41 12 7 22 48 75 -27 43
13 Stoke 40 11 10 19 42 70 -28 43
14 Bournemouth 40 10 12 18 49 68 -19 42
15 Southampton 40 10 12 18 42 56 -14 42
16 West Ham 39 10 11 18 46 69 -23 41
17 West Brom 40 7 14 19 33 56 -23 35
18 Huddersfield 21 6 6 9 18 32 -14 24
19 Brighton 21 5 7 9 15 25 -10 22
20 Hull 19 6 3 10 21 39 -18 21
21 Newcastle 21 5 4 12 19 30 -11 19
22 Middlesbrough 19 1 7 11 10 31 -21 10
23 Sunderland 19 2 4 13 12 34 -22 10

Licha ya kushinda mechi 18 mtawalia, ya mwisho ikiwa dhidi ya Crystal Palace, City hawajafikia rekodi ya kushinda mechi nyingi msimu mmoja.

Wamepungukiwa na mbili kufikia rekodi ya Chelsea waliyoiweka mwaka 2005 waliposhinda mechi 32.

Chelsea walishinda ligi msimu wa 2004-05 na kuhifadhi tena msimu uliofuata.

Haki miliki ya picha Reece Killworth

Harry Kane ndiye hatari zaidi?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kane alifungia Spurs na England mabao 56 katika mechi 52 mwaka 2017

Harry Kane bila shaka yupo kwenye timu nyingi bora za mwaka za mashabiki wengi mwaka 2017.

Ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi mwaka mmoja EPL katika historia, na mwaka 2017 ndiye aliyefunga mabao mengi kwa klabu na timu Ulaya.

Kane alifunga mabao 39 ligini 2017, matatu zaidi ya Alan Shearer alipoweka rekodi ya awali ya EPL 1995.

Alikuwa hatari zaidi Mei na Desemba, ambapo alifunga mabao manane kila mwezi.

Kati ya mabao hayo, kuna hat-trick sita za EPL, ambapo anatoshana na wachezaji wengine wafungaji mabao bora msimu huu EPL.

Hiyo inafikisha jumla ya hat-trick zake hadi nane, zaidi ya zilizofungwa na klabu kadha tangu kuanza kwa EPL.

Kane amefunga hat-trick nyingi zaidi kuwashinda Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Edinson Cavani mwaka huu wote kwa pamoja (ambao walifunga jumla ya hat-trick saba).

Kane alifunga mabao mengi kushinda klabu tatu Ligi ya Premia mwaka 2017.

Haki miliki ya picha Getty Images

Alama zaidi na mabao zaidi

Ukiangazia mwezi kwa mwezi, si ajabu kutambua ni kwa nini Manchester City wamezoa alama nyingi kuliko klabu nyingine tangu Oktoba.

La kushangaza hata hivyo ni kwamba Chelsea haikuzoa alama nyingi mwezi wowote nusu ya pili ya msimu uliopita licha ya kushinda ligi.

Mwezi Alama zaidi
Januari Tottenham (11)
Februari Man City (9)
Machi Liverpool & Bournemouth (7)
Aprili Tottenham (18)
Mei Arsenal (15)
Agosti Man Utd (9)
Septemba Man City (12)
Oktoba Arsenal/Man City (9)
Novemba Man City (12)
Desemba Man City (18)

Na timu iliyofunga mabao mengi zaidi na wachezaji waliofunga mabao mengi zaidi kila mwezi?

Si kila wakati ambapo imekuwa ni Manchester City na Kane.

Mshambuliaji nyota wa Brighton Glenn Murray ni miongoni mwa waliojitokeza.

Mwezi Timu iliyofunga mabao mengi zaidi Mfungaji bora
Januari Tottenham & Arsenal (12) Dele Alli/Harry Kane (5)
Februari Everton (9) Romelu Lukaku (5)
Machi Everton (9) Joshua King/ Lukaku (4)
Aprili Tottenham (16) Son Heung-min/Christian Benteke/Sergio Aguero (5)
Mei Man City & Tottenham (15) Kane (8)
Agosti Man Utd (10) Lukaku/Sadio Mane (3)
Septemba Man City (17) Kane (6)
Oktoba Man City (13) Leroy Sane/Glenn Murray (3)
Novemba Liverpool (11) Mohamed Salah (7)
Desemba Liverpool (20) Kane (8)

Man City wameweka rekodi kwa mabao 102?

Kuna wakati Manchester City walikuwa wanafunga mabao manne au matano katika mechi kila wiki, na wamefunga mabao 102 mwaka wote ligini.

Na tangu kuanza kwa Ligi ya Premia 1993, hakuna klabu nyingine kabla ya City iliyowahi kuzidisha mabao 100.

Mabao mengi yaliyofungwa na timu EPL kwa mwaka
Mwaka Timu Mabao
2017 Man City 102
2016 Liverpool 87
2015 Man City 79
2014 Man City 89
2013 Liverpool 84
2012 Man Utd 90
2011 Man Utd 88
2010 Chelsea 91
2009 Arsenal 86
2008 Chelsea 74
2007 Man Utd/Tottenham 73
2006 Man Utd 79
2005 Chelsea 75
2004 Arsenal 86
2003 Man Utd 79
2002 Arsenal 80
2001 Man Utd 79
2000 Man Utd 95
1999 Man Utd 91
1998 Liverpool 68
1997 Man Utd 83
1996 Man Utd 75
1995 Man Utd 75
1994 Newcastle 84
1993 Man Utd 86

Mwaka mbaya kuwa meneja?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kushoto juu hadi kulia chini: Frank de Boer (Crystal Palace), Craig Shakespeare (Leicester), Paul Clement (Swansea), Ronald Koeman (Everton), Tony Pulis (West Brom) and Slave Bilic (West Ham) wote wamefutwa tangu kuanza kwa msimu

Mwanzo wa msimu huu mameneja sita walimwaga unga kabla ya Krismasi.

Baada ya kufutwa Paul Clement na Swansea kulikuwa na maana kwamba klabu nne ambazo zinavuta mkia ligini zimewafuta mameneja.

Klabu tano kati ya zote zilizowafuta mameneja zimeanza kuboresha matokeo.

Alan Pardew pekee ndiye hajafanikiwa West Brom.

Na mwanzoni mwa mwaka?

Watano walifutwa kabla ya Juni - Mike Phelan (Hull), Claudio Ranieri (Leicester), Aitor Karanka (Middlesbrough), Walter Mazzarri (Watford) na Claude Puel (Southampton).

Kwa jumla, mameneja 11 wamefutwa mwaka 11 Ligi ya Premia, idadi ya juu zaidi katika mwongo mmoja, idadi sawa na ya 2013.

Unaweza kusoma pia:

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii