Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 02.01.2018

Philippe Coutinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Philippe Coutinho

Liverpool itaomba malipo ya juu zaidi kutoka kwa Barcelona kabla ya kufikiria kumuuza kiungo wake wa kati raia wa Brazil Philippe Coutinho. (Telegraph)

Mabingwa hao wa Uhispania wameambiwa kuwa itawagharimu dola milioni 160 kumleta Coutinho huko Nou Camp. (Onda Cero Radio commentator Alfredo Martinez)

Napoli watakuwa tayari kumruhusu beki Faouzi Ghoulam, 23, kuhamia Manchester United kwa pauni milioni 53, wakati wanakamilisha juhudi za kumsaini mchezaji ambaye atachukua mahala pake kwa pauni milioni 26.6 mhispania Alejandro Grimaldo kutoka Benefica. (Record - in Portuguese)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Diafra Sakho

Matumaini ya Chelsea kumshawishi beki raia wa Italia Giorgio Chiellini kuhamia Stamford Bridge, yamepata pigo baada ya kudaiwa kusema kuwa ataongeza mkataba wake na Juventus. (Sky Italia - in Italian)

Swansea wanajaribu kumpata mshambuliaji wa West Ham Diafra Sakho lakini pia watatoa ofa kwa Alfie Mawson 23, au mkorea Ki Sung-yeung,28. (Guardian)

Huddersfield wametoa ofa ya kumsaini mlinzi wa Monaco raia wa uholanzi Terence Kongolo kwa mkopo. (Huddersfield Examiner)

Huddersfield na Watford wanalenga beki wa Wolves Kortney Hause. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden Hazard

Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 120 kwa mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, 26. (Sun)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekana kuwepo tofauti kati ya mshambuliaji Alexis Sanchez, 29, na wachezaji wengine. (Sky Sports)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, amekataa kukana kuwepo jitihada mpya kwa Sanchez baada ya Gabriel Jesus kupata jeraha wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumapili. (Talksport)