Beki wa Liverpool Jon Flanagan akiri kumpiga mpenzi wake England

Jon Flanagan Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jon Flanagan alikiri shtaka baada ya kufikishwa mbele ya mahakimu

Mchezaji wa Liverpool Jon Flanagan amekiri shtaka la kumpiga mpenzi wake.

Beki huyo wa miaka 25 alifika mbele ya hakimu Liverpool Jumanne akishtakiwa kumpiga Rachael Wall.

Alishtakiwa kufuatia kisa cha mnamo 22 Desemba mwendo wa saa 03:20 GMT katika barabara ya Duke katikati mwa mji wa Liverpool.

Atahukumiwa baadaye mwezi huu.

Flanagan ambaye ni mzaliwa wa Liverpool amechezea klabu hiyo mechi zaidi ya 50 tangu alipoanza kuwachezea akiwa na miaka 18.

Mahakama iliambiwa kwamba alionekana kwenye video za CCTV akimpiga mpenzi huyo wake ambaye wamekuwa na uhusiano kwa miezi 18.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Jon Flanagan

Lionel Greig, wakili wa mshtakiwa, aliambia mahakama Flanagan hana historia ya kumpiga mpenzi wake na kwamba wote wawili walikuwa walevi wakati huo.

Hakimu Wendy Lloyd hata hivyo alisema video za CCTV zinamuonesha Flanagan akimpiga mpenzi wake mara kadha.

Flanagan atahukumiwa tarehe 17 Januari.