Arsene Wenger alalamika tena EPL na kupinga mashtaka dhidi yake

Arsene Wenger Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Arsene Wenger

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, amesema atapinga mashtaka yaliyowasilishwa na shirikisho la kandanda la FA baada ya kuibua malalamiko zaidi kwa maafisa kufuatia sare za siku ya Jumatano na Chelsea.

Wenger alikerwa na mwamuzi wa mechi hiyo ya Jumatano Anthony Taylor baada yake kumzawadi Eden Hazard nafasi ya kusawazisha baada yake kuchezewa visivyo na Hector Bellerin.

Wenger alishtakiwa baada ya kukosoa uamuzi wa kuwapa West Brom penalti dakika za mwisho iliyochangia mechi kutoka sare ya 1-1.

Raia huyo wa Ufaransa alikasirishwa na kila alichokitaja kuwa kuipa Chelsea mkwaju wa penalti ambayo ilisababisha mechi kutoka sare ya 2-2.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hector Bellerin alidaiwa kumchezea vibaya Eden Hazard

Akiongea Jumatano Wenger alisema kuwa kwa asilimia 100 atapinga kesi hiyo.

"Mnaweza kusikiliza kila mahojiano niliyoyafanya. Natetea kila kitu nilichokisema bila tatizo lolote," alisema.

Wenger alikasiriwa na na afisa mwingine wakati huu, refa Anthony Taylor, kufuatia uamuzi wa kumpa Eden Hazard fursa ya kusawazishia Chelsea .

Mada zinazohusiana