Ashley Cole aongeza mkataba LA Galaxy

Cole has made 55 appearances for Los Angeles Galaxy Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Cole amechezea Los Angeles Galaxy mechi 55

Beki wa zamani wa England Ashley Cole ameongeza mwaka mmoja kwenye mkataba wake katika klabu ya Los Angeles Galaxy.

Cole, 37, aliojiunga na Galaxy Januari 2016 na amewachezea mechi 55 katika misimu miwili.

Beki huyo wa kushoto wa zamani wa Arsenal na Chelsea alichezea England mechi 107 lakini akafikisha kikomo uchezaji wake timu ya taifa baada ya kukosa kujumuishwa kikosi cha Kombe la Dunia 2014.

Mkufunzi mkuu wa Galaxy Sigi Schmid amesema mchezaji huyo amekuwa "kiongozi muhimu" kwenye timu.

Klabu hiyo itaanza msimu kwa mechi dhidi ya Portland Timbers mnamo 4 Machi.

Mada zinazohusiana