Arsene Wenger achunguzwa tena na FA kuhusu tamko lake juu ya waamuzi

Arsene Wenger Haki miliki ya picha Reuters

Arsene Wenger anakabiliwa na mashtaka zaidi kutoka kwa Chama cha Soka England baada yake kulalamika kuhusu mechi kati ya Arsenal na Chelsea ambayo ilimalizika kwa sare ya 2-2.

Wenger alisema kuna "sadfa ambazo zimezidi" kuhusu maamuzi ya marefa.

Alilalamika kwamba mkwaju wa penalti waliozawadiwa Chelsea wakati wa mechi hiyo Jumatano ulikuwa wa kushangaza sana.

Alisema "hili likirudiwa, inakuwa si sadfa tena".

Wenger tayari amefunguliwa mashtaka ya utovu wa nidhamu kwa kukosoa uamuzi wa refa wa kuwapa West Brom penalti dakika za mwisho katika mechi iliyomalizika kwa sare Jumapili.

Mfaransa huyo alikuwa mepewa hadi 18:00 GMT kujibu mashtaka kufuatia pia vitendo vyake ndani ya chumba cha kubadilishia mavazi cha waamuzi Hawthorns baada ya Calum Chambers kudaiwa kunawa mpira eneo la hatari na mwamuzi Mike Dean.

Huku mechi ikiwa imesalia dakika moja kumalizika The Hawthorns, Arsenal wakiongoza 1-0, Calum Chambers aliadhibiwa baada ya Kieran Gibbs kuusukuma mpira na ukagusa mkono wake.

Wenger alihisi kwamba mchezaji huyo hakuunawa mpira huo makusudi.

Sheria za soka zinasema adhabu inafaa kutolewa tu iwapo mchezaji alinawa mpira makusudi na kwamba umbali kati ya mchezaji mpinzani na mpira unafaa kuzingatiwa.

Chambers alikuwa amesimama mita mbili hivi kutoka kwa Gibbs.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hector Bellerin alidaiwa kumfanyia madhambi Eden Hazard

Wenger alisema bila shaka atapinga mashtaka hayo asilimia 100 na kusema: "Mnaweza kusikiliza kila mahojiano niliyoyafanya. Nasisitiza kila jambo nililolisema bila tatizo."

Arsenal waliadhibiwa tena dakika za mwisho dhidi ya Chelsea pale Eden Hazard alipoanguka eneo la hatari baada ya kukabiliwa na Hector Bellerin.

Wenger amepewa hadi 18:00 GMT Jumanne on Tuesday, 9 Januari kujibu mashtaka kuhusu aliyoyasema kabla na baada ya mechi.

"Lazima niseme kwamba kilichonisikitisha zaidi ni kwamba hili limetokea mara nyingi msimu huu - Stoke, Watford, Manchester City, West Brom," alisema Wenger Jumanne.

"Hii ni sadfa ambayo inanitia wasiwasi."

Januari, alipigwa marufuku kutokuwa uwanjani mechi nne baada ya kupatikana na hatia kumhusu mwamuzi Anthony Taylor mechi ya ligi dhidi ya Burnley.

Mada zinazohusiana