Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 07.01.2018

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Riyad Mahrez

Liverpool wana nia ya kumsaini Riyad Mahrez huku mshambuliaji huyo wa Leicester City raia wa Algeria akitarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya leo Jumapili. (Bein Sports)

Liverpool wako tayari kufanya hima kujaza pengo lilioachwa na Philippe Coutinho ambaye ameelekea Barcelona huku wing'a wa Monaco Thomas Lemar 22, akiwa nambari moja katika orodha yao.

Haki miliki ya picha Empics
Image caption Alexis Sanchez

Manchester City wanatarajiwa kutoa ofa ya paunia milioni 25 kwa mchezaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, 29, lakini hatua hatua hiyo itafikisha kikomo mbio za kumtafuta mlinzi wa Real Sociedad, Inigo Martinez. (Sunday Mirror)

Ciy pia wanamwinda mlinzi wa Leicester Harry Maguire, 24, na wanaweza kutoa ofa ya pauni milioni 50 kwa kiungo huyo wa kati wa zamani wa Hull City. (Sun on Sunday)

Manchester United huenda wakajaribu kumleta Gareth Bale kutoka Real Madrid, kabla ya msimu wa kununua wachezaji wapya kukamilika. (Sunday Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gareth Bale

Arsenal wanakabiria kuafikia makubalianoa ya pauni milioni 25 kwa kiungo wa kati wa West Brom raia wa Ireland Kaskazini Jonny Evans, 30. (Sun on Sunday)

Meneja Mauricio Pellegrino anasema Southampton wana matumaini ta kumsaini wing'a wa Arsenal na England Theo Walcott, 28. (ESPN)

Meneja wa Bayern Munich, Jupp Heynckes amekana madai ya kumuuza kiungo wa kati raia wa Chile Arturo Vidal kwenda Chelsea mwezi Januari (Mail on Sunday)

Mada zinazohusiana