Coutinho asema kutua Barca ndoto zimetimia

base Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Philippe Coutinho amesema uhamisho wake kwenda Barcelona ni ndoto iliyokamilika

Kiungo wa kibrazil Philippe Coutinho amesema uhamisho wake kwenda Barcelona ni ndoto iliyokamilika.

Kiungo huyo alieleza hisia zake za kutimiza ndoto yake alipokuwa akipigwa picha katika uwanja wa Nou Camp wakati klabu yake mpya ilipokuwa ikicheza na Levante.

"Mashabiki wa Barcelona tayari nipo hapa, ndoto zimekuwa kweli natumani tunaonana kesho, " alisema Coutinho kupitia video fupi aliyoiweka katika mtandao wa Twita.

Coutinho anatarajiwa kutambulishwa leo kuwa mchezaji mpya wa Barcelona baada ya klabu yake ya Liverpool kukubali kuuza kiungo huyo kwa dau la pauni milioni 142.

Nyota huyu atasaini mkataba wa miaka mitano na klabu itayotaka kumnunu mchezaji huyo italazimika kutoa kiasi cha pauni milioni 355.

Mada zinazohusiana