Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 08.01.2018

Antoine Griezman Haki miliki ya picha AFP
Image caption Antoine Griezman

Mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 26, ataitisha pauni 400,000 kwa wiki kuzuia ofa ya Chelsea ili kujiunga na Manchester United. (Sun)

Chelsea wanamtaka mshambuliaji wa Borussia Monchengladbach na Ubelgiji Thorgan Hazard, 24, kujiunga na ndugu zake Eden, 27, na Kylian, 22, huko Stamford Bridge. (Bild - in German)

Liverpool wanamtaka mshambuliaji wa Monaco na Ufaransa Thomas Lemar, 22, kuchukua mahala pake Philippe Coutinho - na wanataka kufanya hilo wiki hii. (Mirror)

Manchester United na Chelsea zimemuulizia mshambuliaji wa Porto Mousa Marega, 26. (Metro)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Thomas Lemar

Real Madrid walikuwa na nia ya kutoa ofa ya pauni milioni 177 kwa Coutinho kabla ya kukubali kujiunga na Barcelona kwa pauni milioni 142. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Coutinho atafanyiwa uchunguzi wa kiafya leo Jumatatu na kutangazwa rasmi kama mchezaji wa Barcelona lakini kuanza kwake kucheza kunaweza kucheleweshwa kutokana na jeraha.

Nyota wa Barcelona Lionel Messi ametaka Philippe Coutinho kuwepo katika kikosi cha kwanza badala ya Ousmane Dembele. (Diario Gol)

Haki miliki ya picha Robbert MICHALE/GETTY IMAGES
Image caption Naby Keita

Liverpool watajaribu kumleta kiungo wa kati wa RB Leipzig na Guinea Naby Keita Anfield na wana nia ya kulipa zaidi kumpata mchezaji huyo wa miaka 22 mwezi Januari. (Telegraph)

Wing'a mbrazil Lucas Moura, 25, anataka kuondoka Paris St-Germain kujiunga na Manchester United mwezi huu. (Telefoot via Express)

Real Madrid inapanga kuwasajili Eden Hazard, 27 na kipa Thibault Courtois, 25, kutoka Chelsea ifikapo mwisho wa msimu. Lakini watasubiri kuona hatma ya Harry Kane wa Tottenham. (Sky Sports)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anasema klabu yake haiko tayari kuongeza wachezaji zaidi Januari baada ya kumnunua kijana kutoka Ugiriki wa umri wa miaka 20, Konstantinos Mavropanos. (Sun)

Bournemouth wanatarajiwa kumsaini mfungaji bora zaidi wa Colchester United, Sammie Szmodics, 22, kwa gharama ya pauni milioni moja.

Kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk na Brazil Fred, 24, anasema anasubiri simu kutoka kwa meneja wa Manchester City Pep Guardiola. (GloboEsporte, kupitia Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pep Guardiola

NewCastle wana matumaini ya kumaliza kumsaini wing'a wa Chelsea mbrazil Kenedy, 21. (Newcastle Chronicle)

Leicester City wakaribia kumsaini mchezaji wake wa kwanza mwezi Januari - mshambuliajo wa Mali Fousseni Diabate.

The Foxes wamekubalia pauni milioni 1.7 kwa mchezaji huyo wa miaka 22 ambaye anacheza ligi ya pili ya Ufaransa Gazelec Ajaccio. (Leicester Mercury)

Leeds United wamemurodhesha beki wa Brugge ya Ubelgiji Laurens de Bock, 25, kuwa lengo lake kuu. (Leeds Live)

Mwanariadha nguli Usain Bolt, 31, amesema atafanya majaribio na Borussia Dortmund mwezi Machi, lakini anatamani sana kuichezea Manchester United. (Express)

Mada zinazohusiana