Jonny Evans: Arsenal na Man City washindania beki wa West Brom

West Brom defender Jonny Evans Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja mpya wa West Brom Alan Pardew amesema klabu hiyo itamuuza tu iwapo itapata 'ofa bora zaidi'

Arsenal na Manchester City wanataka kumnunua beki ambaye pia ni nahodha wa West Brom Jonny Evans.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaaminika kuwa tayari kuomba klabu yake kutoa £25m kumnunua mchezaji huyo wa miaka 30 kutoka Ireland Kaskazini.

Arsenal wana nafuu kidogo kwani West Brom wanamtaka beki wa kushoto Mathieu Debuchy, 32, ambaye anatafuta fursa ya kuchezwa kikosi cha kwanza.

City wanataka mchezaji wa kujaza nafasi ya nahodha Vincent Kompany ambaye ameumia tena.

Klabu nyingine za Ligi ya Premia pia zinamtaka Evans lakini haziwezi kushindana na klabu ambazo zinacheza soka ya Ulaya.

Evans alijiunga na West Brom kutoka Manchester United kwa £6m Agosti 2015.

Mada zinazohusiana