Droo Kombe la FA: Manchester United wapewa Yeovil Town

Yeovil Town v Manchester United in 2015 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester United walilaza Yeovil katika Kombe la FA mwaka 2014-15

Klabu ya Yeovil Town inayocheza ligi ya daraja la tatu, ambayo ndiyo klabu ya ngazi ya chini zaidi iliyosalia katika Kombe la FA msimu huu, imepangwa kukutana na mabingwa mara 12 wa kombe hilo Manchester United raundi ya nne.

Tottenham pia watakutana na klabu ya League Two, Newport County.

Viongozi wa Ligi ya Premia Manchester City wamepangwa kukutana na mshindi kati ya Cardiff City na Mansfield.

Nottingham Forest, ambao waliwaondoa mabingwa watetezi Arsenal Jumapili watakutana na wenzao wa ligi ya Championship Hull City.

Mechi za raundi ya nne zitachezwa wikendi ya 26-29 Januari.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Yeovil wanashikilia nafasi ya 21 katika League Two

Droo kamili raundi ya nne:

Liverpool v West Brom

Peterborough v Fleetwood/Leicester

Huddersfield v Birmingham

Notts County v Wolves/Swansea

Yeovil v Manchester United

Carlisle/Sheffield Wednesday v Stevenage/Reading

Cardiff/Mansfield v Manchester City

MK Dons v Coventry

Millwall v Rochdale

Southampton v Watford

Middlesbrough v Brighton/Crystal Palace

Bournemouth/Wigan v Shrewsbury/West Ham

Hull v Nottingham Forest

Newport County v Tottenham

Norwich/Chelsea v Newcastle

Sheffield United v Preston

Mada zinazohusiana