Chelsea na Arsenal kukabiliana nusu fainali ya Carabao

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard atashiriki mechi hiyo
Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard atashiriki mechi hiyo

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard atashiriki katika mechi dhidi ya Arsenal katika awamu ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la Carabao siku ya Jumatano baada ya kupona jereha.

Mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa pauni milioni 15 kutoka Everton Ross Barkley hatoshiriki kwa kuwa bado anauguza jereha la nyuma ya goti.

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ataendelea na marufuku ya kutokalia eneo la wakufunzi uwanjani na badala yake kukaa katika viti vya mashabiki huku kikosi chake kikirudi baada ya kufungwa na klabu ya Nottinham Forest katika kombe la FA.

Granit Xhaka anauguza jeraha la kinena huku Shkodran Mustafi ambaye aligongwa akiwa hajulikani iwapo atashiriki.

Mfumo wa kiteknolojia wa video ya kumsaidia refa VAR utatumika katika awamu zote mbili za nusu fainali hiyo.

Arsenal haijashinda kombe hilo kwa kipindi cha miaka 25 huku Chelsea ikiweza kushinda mara ya mwisho 2015.