Pep Guardiola aweka rekodi ya meneja bora EPL, Harry Kane pia atamba

Guardiola surpassed Antonio Conte's mark of three consecutive wins Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Guardiola amempita Antonio Conte aliyekuwa ameshinda miezi mitatu mtawalia

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameweka rekodi mpya Ligi ya Premia kwa kutawazwa meneja bora wa mwezi mara nne mtawalia.

Guardiola, 46, ametawazwa meneja bora wa mwezi Desemba baada ya klabu yake kushinda mechi sita ligini na kutoka sare mechi moja.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte alikuwa anashikilia rekodi ya awali, kwa kutawazwa meneja wa mwezi mara tatu mtawalia mwaka 2016.

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ndiye aliyekuwa mchezaji bora wa Desemba, ambapo amefikia rekodi ya kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard ambaye alikuwa ameshinda tuzo hiyo mara sita.

Kane, 24, alifunga mabao manane - ikiwa ni pamoja na hat-trick mbili- mwezi Desemba.

Klabu yake ya Spurs ilishinda mechi nne na kutoka sare moja. Walishindwa mechi moja na City ambao hawajashindwa Ligi ya Premia msimu huu na wamo alama 15 mbele kileleni.

Mada zinazohusiana