Manchester City kukosa huduma za Alexis Sanchez huku United ikimnyatia

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger
Image caption Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger

Manchester City huenda ikamkosa Alexis Sanchez ambaye sasa inadaiwa anaelekea Manchester United - badala ya kuilipa Arsenal dau la £35m.

Pia inaaminika kwamba ajenti wa Sanchez anataka dau la £5m kama malipo yake katika makubaliano hayo hivyobasi kufanya dau hilo kupanda hadi £40m -ikiwa ni maradufu ya fedha ambazo City iko tayari kulipa.

Sanchez, 29, ataondoka Arsenal mnamo mwezi Januari iwapo ombi la kuvutia litawasilishwa huku Arsenal wakipata mchezaji wa kuchukua mahala pake.

Mkufunzi wa United Jose Mourinho alisema kuwa Sanchez ni mchezaji muhimu siku ya Ijumaa.

"Sanchez ni mchezaji wa Arsenal ," Mourinho aliongezea. Sijui, lakini hii wikendi ataichezea Arsenal, kwa hivyo sidhani kwamba ni sawa kuzungumza kuhusu Alexis Sanchez.

"Mimi binafsi, bodi ya Manchester United na wamiliki wa klabu hatuamini mambo mengi katika uhamisho wa mwezi Januari. Hatuamini kumsajili mchezaji bila mpango.

"Kile tunachoamini ni kwamba kuna wachezaji katika ulimwengu wa soka ambao iwapo una fursa ya kuwasajili mwezi Januari , Machi ama Julai unalazimika kujaribu .

Haki miliki ya picha you tube
Image caption Alexis Sanchez

Klabu ya PSG pia wamehusishwa na uhamisho wa mshambuliaji huyo wa Chile lakini Sanchez anapendelea kuhamia Manchester City.

Lakini huku goti la Gabriel Jesus likionekana kutokuwa na jeraha baya sana kama ilivyohofiwa , mkufunzi wa City Pep Guardiola alisema siku ya Alhamisi kwamba mshambuliaji huyo wa Brazil huenda akarudi hivi karibuni katika kipindi cha wiki mbili au tatu -klabu hii haioni ni kwa nini ilipe dau kubwa kwa mchezaji ambaye atakuwa huru mwisho wa msimu.

Mada zinazohusiana