Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 13.01.2018

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez mwezi Januari , akisema mchezaji huyo, 29 anaweza kuwa ''uwekezaji mzuri''. (Telegraph)

Tottenham iko tayari kufutilia mbali hamu ya kutaka kumsajili winga wa Bordeaux Malcom kwa sababu klabu hiyo ya Ufaransa inaitisha dau la £45m ili kumunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20- ijapokuwa Arsenal bado ina hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa Brazil (Mail)

Tottenham iko tayari kuanza mazungumzo ya malipo ya mshambuliaji Harry Kane, 24, huku ikijiandaa kumuongezea kandarasi kiungo wa kati Christian Eriksen, 25, na mshambuliaji Son Heung-min, 25. (Times - subscription required)

Manchester United inapanga kuanza mazungumzo ya kumuongezea kandarasi kipa David de Gea ambayo yatamfanya kipa huyo kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika klabu hiyo akipata £300,000 kwa wiki. (Sun)

Manchester United hawana sababu ya kumsaka mshambuliaji wa Leicester waliyekuwa na hamu naye Jamie Vardy, 30. (Leicester Mercury)

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa mazungumzo kuhusu mkataba mpya na kiungo wa kati Mesut Ozil, 29, yanaendelea huku kukiwa na matumaini kwamba huenda akasalia na The Gunners.(Telegraph)

Manchester City wamewasilisha ombi la £45m kumsajili mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk raia wa Brazil Fred, 24. (Manchester Evening News)

Klabu ya Uhispania ya Espanyol imejiandaa na kuondoka kwa mkufunzi wake Quique Sanchez Flores ambaye anaelekea Stoke City. (Marca - in Spanish)

Mkufunzi wa West Ham David Moyes anataka dirisha la uhamisho la mwezi Januari kuwa wazi kwa juma moja pekee huku siku ya mwisho ikiwa sawa kama ile ya Itali, ambapo hufanyika katika Hoteli ambapo vilabu na maajenti hukutana ili kukamilisha mikataba (Times - subscription required)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Manchester United na Uholanzi Robin van Persie, 34, anatarajiwa kuondoka katika klabu ya Uturuki ya Fenerbahce kujiunga na klabu ya Uholanzi ya Feyenoord - ambapo alianza kusakata soka ya kulipwa. (AD - in Dutch)

Chelsea wana hamu ya kumuajiri mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri au mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri kuwa mrithi wa mkufunzi Antonio Conte. (Evening Standard)

Kandarasi ya mchezaji wa Argentina Lionel Messi na klabu ya Barca inamfanya yeye kulipwa zaidi ya Yuro milioni 100 kwa mwaka katika mshahara.(Mediapart - in French, subscription required)

Real Madrid walikuwa tayari kumlipa Messi mwenye umri wa miaka 30 250m euro (£221.7m) kama fedha za kumnunua 2013. (El Mundo - in Spanish)

Nottingham Forest, Aston Villa, Leeds United na Cardiff City wanataka kumsajili Kiungo wa kati wa Middlesbrough's ,28, na Uingereza Adam Clayton. (Northern Echo)

Mkufunzi wa Middlesbrough Tony Pulis anataka kumsajili mchezaji mmoja ama wawili mwezi huu lakini anasema kuwa kikosi chake tayari kina wachezaji wengi.. (Evening Gazette)

Sunderland inataka kumsajili mshambuliaji wa Burnley ,34, na Jamhuri ya Ireland Jon Walters kwa mkopo hadi mwisho wa msimu(Northern Echo)

Mshambuliaji wa Crystal Palace, 29, na Mali Bakary Sako anataka kusalia katika klabu hiyo licha ya kandarasi yake kukamilika mwisho wa msimu huu. (Croydon Advertiser)

Schalke Inataka kumsajili kwa mara nyengine beki wa Chelsea Baba Rahman. Mchezaji huo mwenye umri wa miaka 23 na raia wa Ghana alihudumumia nusu ya kwanza ya msimu uliopita akicheza kwa mkopo katika klabu hiyo ya Ujerumani. (Evening Standard)Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi alilipa kodi ya zaidi ya Yuro 12m (£10.64m) mwishoni mwa 2016 ili kuzuia adhabu zaidi inayotokana na maswala yake ya kifedha , na fedha hizo alirejeshewa na klabu yake(Der Spiegel)

Mada zinazohusiana