Kijana wa miaka 20 ajishindia $451m kwa bahati nasibu Marekani

Bwana Missler akipiga picha na dadake. Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Bwana Missler akipiga picha na dadake.

Kijana wa miaka 20 mjini Florida nchini Marekani anasema kuwa anapanga kujifurahisha baada ya kutangazwa mshindi wa $451m katika mchezo wa bahati nasibu.

Shane Missler alifananisha nambari tano na mpira wa bonassi ili kujishindia zawadi hiyo ambayo ni ya nne kwa ukubwa katika historia ya mchezo huo nchini Marekani.

Alitarajiwa kulipwa malipo ya kwanza ya $282 badala ya fedha zote kwa kipindi cha mda mrefu.

Bwana Missler alisema alikuwa na hisia kwamba ataibuka mshindi mkesha wa usiku wa droo hiyo ya mamilioni ya dola.

Dakika chache baadaye droo hiyo wiki moja iliopita alichapisha ujumbe katika mtandao wake wa facebook: Oh My God.

Bwana Missler aliwasilisha tiketi yake ya ushindi katika makao makuu ya mchezo huo wa bahati nasibu katika eneo la Tallahassee siku ya Ijumaa akiandaman na babake na wakili.

Haki miliki ya picha facebook
Image caption Shane Missler kabla na baada ya kushinda jackpot

Amesema kuwa ana mipango mikubwa na fedha hizo.Nina miaka 20 pekee.

''Lakini natumai kutumia kufuatilia mambo yangu ya kibinafsi niliotaka kufanya, kusaidia familia yangu mbali na kusaidia jamii'', alisema bwan Missler kulingana na taairfa hiyo.

Mada zinazohusiana