Bournemouth wawalima Arsenal 2-1

Callumn Wilson scores Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bournemouth 2-1 Arsenal

Kipindi kigumu cha Arsenal kiliendelea baada ya mabao kutoka kwa Callum Wilson na Jordon Ibe kuiwezesha Bournemouth kutoka nyuma na kuwashinda kwa mabao 2-1.

Sasa kikosi cha Arsene Wenge kina mechi tano bila ushindi na kubaki nyumba kwa pointi tano wakati Bournemoutha wakiendelea na mechi nne bila ya kushindwa.

Mlinzi Hector Bellerin aliwapatia wageni waliocheza bila ya Alexis Sanchez, uongozi wakati Alex Iwobi alipomimina kombora kumzidi Asmir Begovic.

Lakini Wilson alitumia fusra ya makosa yake Petr Cech na kutumbukiza mpira wavuni.

Upande wa Eddie Howe ulipata ushindi wa kwanza kabisa dhidi ya Arsenal na kupanda hadi nafasi ya 13 na pointi 4 kutoka hatarini.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bournemouth 2-1 Arsenal

Mada zinazohusiana