Manchester United huenda wakamchukua Alexis Sanchez

Alexis Sanchez Haki miliki ya picha PA

Manchester United wana nafasi nzuri sana ya kumnunua Alexis Sanchez kutoka kwa klabu yake ya Arsenal.

Hii ni baada ya habari kuibuka kwamba wako tayari kulipa £35m, ambazo ndizo pesa ambazo Arsenal wamekuwa wakitaka kulipwa kumwachilia.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alisema Jumapili kwamba mustakabali wa Sanchez utaamuliwa katika kipindi cha saa 48 zijazo.

Hii ni baada yake kumwacha nje ya kikosi ambacho kilicheza mechi ambayo Arsenal walilazwa 2-1 na Bournemouth Ligi ya Premia.

Sanchez alitaka sana kwenda Manchester City lakini hali kwamba United wako tayari kutimiza matakwa ya mchezaji na klabu inaifanya rahisi kwake kumchukua.

Inaarifiwa kwamba Arsenal wanamtaka pia mchezaji wa United kutoka Armenia Henrikh Mkhitaryan.

Mkataba wa Sanchez unafikia kikomo mwisho wa msimu na alikaribia sana kujiunga na City kwa £60m siku ya mwisho ya kuhama wachezaji Agosti mwaka jana, lakini uhamisho wake ukatibuka baada ya Arsenal kushindwa kumnunua kiungo wa kati wa Monaco na Ufaransa Thomas Lemar.

Meneja wa United Jose Mourinho alisema Ijumaa kwamba Sanchez ni "mchezaji mzuri sana".

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mkataba wa Sanchez Arsenal unamalizika mwisho wa msimu

Aliongeza: "Tunachokiamini ni kwamba tuna wachezaji fulani katika ulimwengu wa soka ambao ukapata fursa ya kuwanunua Januari, Machi au Julai, lazima ujaribu. Na ni hivyo."

Meneja wa City Pep Guardiola angetaka sana kumnunua mchezaji huyo aliyefanya kazi naye Barcelona na bado kuna matumaini kwamba City wanaweza kurejea na ofa nyingine na kubadilisha mambo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii