Paul Lambert ateuliwa meneja Stoke City

Paul Lambert Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lambert mara ya mwisho alifanya kazi Wolverhampton Wanderers

Stoke City wamemteua meneja wa zamani wa Aston Villa na Norwich Paul Lambert kuwa meneja wao mpya.

Raia huyo wa Scotland wa umri wa miaka 48 ametia saini mkataba wa miaka miwili unusu.

Atachukua usukani kutoka kwa Mark Hughes aliyefutwa kazi mwezi uliopita.

Stoke wamo nafasi ya 18 katika Ligi ya Premia, wakihitaji alama moja kuwa salama, na waliondolewa kutoka michuano ya Kombe la FA na Coventry City.

Lambert atafuatilia mechi yao ya Jumatano dhidi ya Manchester United (20:00 GMT) akiwa sehemu ya mashabiki na atachukua rasmi mikoba Jumanne.

Mechi yake ya kwanza kwenye usukani itakuwa mechi ya nyumbani dhidi ya Huddersfield Jumamosi.

Haki miliki ya picha Getty Images

Lambert amekuwa bila kazi tangu kuondoka klabu ya Wolves mwishoni mwa msimu uliopita.

Amewahi kuwa mkufunzi Colchester, Wycombe Wanderers na Blackburn.

Alipokuwa mchezaji, alishinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Borussia Dortmund mwaka 1997 na akashinda mataji manne ya ligi Scotland akwia na Celtics.

Alichezea timu ya taifa ya Scotland mechi 40.

Mada zinazohusiana