Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 16.01.2018

Pierre-Emerick Aubameyang Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pierre-Emerick Aubameyang

Arsenal wako kwenye mazungumzo kumsani mchezaji wa Borussia Dortmund na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kuchukua mahala pake Alexis Sanchez. (Mirror)

Arsenal wako mbioni na pauni milioni 53 kumpata Aubameyang 28. (Mail)

Na Jose Mourinho anasema kuwa hana ukakika kuwa atamleta Sanchez huko Manchester United. (Mirror)

Chelsea pia wamejiunga katika mbio za kumpata Sanchez lakini United wana uhakika kuwa kumpeana Henrikh Mkhitaryan, 28, kama sehemu ya makubaliano inawaweka katika nafasi nzuri. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo, 32, anataka kurudi Manchester United. (As.com - in Spanish)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Cristiano Ronaldo

Kiungo wa kati Emre Can, 24, anasema kuwa hajasaini makubaliano ya kujiunga na Juventus msimu huu na bado anazungumza na Liverpool kuhusu kuendelea kubaki huko Anfield. (Times - subscription required)

Swansea City wamefanya mazungumzo na Atletico Madrid kuhusu makubaliano ya kuwaleta mshambuliaji wa raia wa Ufaransa Kevin Gameiro 30, na mBrazil Nicolas Gaitan, 29, huko south Wales Januari hii. (Wales Online)

Everton wanajaribu kukamilisha makubaliano ya pauni milioni 20 kwa wing'a wa Arsenal na England Theo Walcott 28, wiki hii. (Mirror)

Bournemouth nao wamewajulisha Arsenal kuhusu kumchukua Walcott kwa mkopo kwa msimu wote. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Walcott

Sevilla wana uhakika wa kumpata kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi, 24. (ESPN)

Meneja wa Wales Ryan Giggs anatathmini hatua ya kumfanya mchezaji mwenza katika Manchester United Paul Scholes kuwa mmoja wa kikosi chake. (Mail)

Mtaalamu wa masuala ya kandanda mfaransa Julien Lauren ana uhakika kuwa mshambulia wa PSG mBrazil Neymar 25, na mchezaji aliye kwenyr mkopo raia wa Ufaransa Kylian Mbappe, 19, wakati mmoja watakuwa wachezaji wa Real Madrid. (BBC Radio 5 live)

West Brom wanatoa ofa ya pauni milioni 12 kwa kiungo wa kati wa Fulham Tom Cairney, 26. (Sun)

Birmingham City wanataka kumsani beki wa Feyenoord Miquel Nelom, 27. (Mail)

Haki miliki ya picha Empics
Image caption Alexis Sanchez

Arsenal wako makini kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan 28, kama sehemu ya makubaliano ambayo yatamleta mshambuliaji raia wa Chile Alexis Sanchez, 29, huko Old Trafford. (Guardian)

Manchester City wamejitoa katika makubaliano ya kumsaini Sanchez na pesa zilizoitishwa na ajenti wake. (Goal)

Arsenal ilifanya mazungumzo na mshambuliaji wa Bordeaux Malcom siku ya Jumapili na wanatarajia kulipa pauni milioni 40 kwa mBrazil huyo wa miaka 20. (Guardian)

Arsenal na Chelsea wanammezea mate mshambuliaji wa Watford raia wa Brazil Richarlison 20. (Sun)

Mada zinazohusiana