Ronadinho astaafu kucheza soka

Ronadinho astaafu kucheza soka
Image caption Ronadinho astaafu kucheza soka

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na klabu za PSG, Barcelona na Ac Milan Ronaldo de Assis Moreira Maarufu kama Ronadinho Gaucho amestaafu soka.

Licha ya Ronadinho kutocheza soka la kiushindani toka mwaka 2015 amekuwa akicheza michezo ya mabonanza

Kaka na wakala wa mchezaji huyo Roberto Assis amethibitisha kuwa umefika mwisho kwa fundi huyo wa Brazil kucheza soka.

Ronaldinho alianzia soka yake katika klabu ya Gremio ya nchini kwao kabla ya kujiunga na Paris St-Germain mwaka 2001 na baadaye kujiunga na Barcelona alikong'ara sana.

Katika msimu wa 2010 -2011 alijiunga na AC Milan ya Italia kabla ya kurudi kwao na kujiunga na Flamengo mwaka 2011. Kisha alichezea vilabu vya Atletico Mineiro, na Queretaro ya nchini Mexico na kurudi tena kwao Brazil katika klabu ya Fluminense.

Mada zinazohusiana