Mchezaji anayelengwa na Arsenal aicheka timu yake baada ya kufungwa

Mchezaji anayelengwa kusajiliwa na Arsenal katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari Malcom anakabiliwa na kesi ya utovu wa nidhamu katika klabu ya Bordeaux.g Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji anayelengwa kusajiliwa na Arsenal katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari Malcom anakabiliwa na kesi ya utovu wa nidhamu katika klabu ya Bordeaux.

Mchezaji anayelengwa kusajiliwa na Arsenal katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari Malcom anakabiliwa na kesi ya utovu wa nidhamu katika klabu ya Bordeaux.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alionyeshwa katika mitandao ya kijamii akicheka na kufanya utani pamoja na wachezaji wenza Cafu na Otavio baada ya timu yao kushindwa na klabu ya Caen siku ya Jumanne.

Bordeaux waliomsajili mchezaji huyo wa Brazil kutoka Corinthians 2016 ilisema kuwa wachezaji hao walionyesha ukosefu wa ukomavu, umoja na heshima kwa taasisi hiyo.

Klabu hiyo ilisema kuwa inashutumu vikali kanda ya video na kwamba mashtaka ya kuwachukulia adhabu yataanzishwa.

Malcolm amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal kutoka Bordeaux ambapo amefunga magoli 18 katika mechi 80.

Hatahivyo makubaliano yoyote yataafikiwa iwapo mshambuliaji wa Gunners Theo Walcot atajiunga na Everton.

Arsenal pia inamtaka kiungo wa kati wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan na mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang na haiwezekani kwamba watawasajili wachezaji wote watatu.

Mada zinazohusiana