Paul Pogba ni mbunifu zaidi uwanjani kuliko Kevin De Bruyne

Mchezaji wa ManCity Kevin De Bryune na mwenzake wa man United Paul Pogba huku raheem sterling akiangalia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji wa ManCity Kevin De Bryune na mwenzake wa man United Paul Pogba huku raheem sterling akiangalia

Paul Pogba ana mchezo wenye ubunifu zaidi ya kiungo wa kati wa Manchester City Kevin De Bruyne, kulingana na takwimu.

Mchezaji huyo wa Manchester City amekuwa akionyesha mchezo mzuri katika kikosi cha Pep Guardiola msimu huu.

Lakini ni kiungo wa kati wa Manchester United aliyevunja rekodi ya usajili ambaye amefaa zaidi uwanjani.

Pogba ametoa pasi tisa za magoli katika mechi 13 za Man United.

De Bruyne amefanikiwa kutoa pasi kama hizo lakini katika mechi 23.

Usaidizi wa pasi zinazotolewa na Pogba ili kupata magoli ni mzuri zaidi ya mchezaji yeyote yule katika ligi tano za bara Ulaya msimu huu.

  • Paul Pogba (Man Utd) - Pasi 9 katika mechi 13
  • Neymar (PSG) - Pasi 9 katika mechi 14
  • Philipp Max (Augsburg) - Pasi 9 katika mechi 18
  • Pione Sisto (Celta Vigo) - Pasi 9 katika mechi 19
  • Leroy Sane (Man City) - Pasi 9 katika mechi 21
  • Kevin De Bruyne (Man City) - Pasi 9 katika mechi 23

Kevin De Bryune ametoa usaidizi kama huo wa Pogba lakini katika mechi 10 zaidi.

Neymar anamfuata Drogba katika jedwali la kutoa pasi zilizozaa magoli.

Hatahivyo, licha ya Pogba kuwasaidia wachezaji wenzake , ni safu ya mashambulizi ya Manchester United ambayo imekifanya kikosi cha Jose Mourinho kuwa nyuma ya Manchester City kwa pointi 12.

Antonio Valencia, Anthony Martial na Romelu Lukaku wote walifunga wakati United ilipoicharaza stoke City mabao 3-0.

Pogba alihusika katika kutoa pasi ya bao lililofungwa na Valencia kunako dakika ya tisa na bao la Martial dakika ya 29 baadaye.

Kwa jumla msimu huu City imefunga mabao 67 huku majirani zao wakifunga magoli 48.

Mada zinazohusiana