Neymar amnyima Cavani fursa ya kuwa na mabao mengi katika historia ya PSG

Neymar alizomwa na mashabiki wa Paris St-Germain baada ya kumnyima Edinson Cavani fursa ya kuwa mchezaji aliyeifungia klabu hiyo mabao mengi wakati wa mechi dhidi ya Dijon
Image caption Neymar alizomwa na mashabiki wa Paris St-Germain baada ya kumnyima Edinson Cavani fursa ya kuwa mchezaji aliyeifungia klabu hiyo mabao mengi wakati wa mechi dhidi ya Dijon

Neymar alizomewa na mashabiki wa Paris St-Germain baada ya kumnyima Edinson Cavani fursa ya kuwa mchezaji aliyeifungia klabu hiyo mabao mengi wakati wa mechi dhidi ya Dijon.

Bao la kipindi cha kwanza la Cavani lilimfanya kuwa sawa kwa magoli na mshambuliaji wa zamani Zlatan Ibrahimovic akiwa na magoli 156 katika mashindano yote aliyochezea PSG.

Wenyeji hao waliongoza kwa 4-0 katika kipindi cha kwanza na Neymar alikuwa tayari amekamilisha hat-trick kabla ya PSG kupata penalti.

Hatahivyo raia huyo wa Brazil aliamua kupiga mkwaju huo wa penalti badala ya kumwachia Cavani, hatua iliomfanya Neymar kuzomwa na mashabiki wa timu hiyo , lakini kocha Unai Emery alimtetea mchezaji huyo baada ya mechi hiyo.

Image caption Neymar na Cavani wakishindana ni nani anayefaa kupiga penalti

''Nadhani Neymar alipiga mkwaju huo wa penalti kwa sababu ilikuwa siku nzuri kwake'', alisema Emery.

''Tunafurahia. Lakini kutakuwa na fursa nyingi kwa Cavani kufunga mabao zaidi''.

Beki wa PSG Thomas Meunier aliitaja hatua hiyo ya Neymar kuwa aibu lakini akaongezea kuwa ni Neymar aliyepewa jukumu la kupiga penalti.

''Angempatia mpira ingekuwa ishara nzuri ya fair Play'', alisema.

''Aliifanyia kazi kubwa timu yetu na swala la kuzomwa na mashabiki , kwa kweli hakuipiga vizuri. Nadhani wachezaji wengi wangefanyiwa hivyo''.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Mshambuliaji wa PSG Edinson Cavani

PSG inaongoza kwa pointi 11 kutoka kwa wapinzani wake wa karibu Lyon baada ya mechi 21.

Vionghozi hao wa ligi wameshinda mechi nane zilizopita na michuano ya kuwania mataji, wakiwa wamefunga mabao 31 na kufungwa sita pekee.

Dijon ambao wako katika nafasi ya 11 katika jedwali hawajashinda hata mechi moja katika mechi nne walizocheza.

Mada zinazohusiana