Jose Mourinho: Ninasubiri habari njema za kumsajili Alexis Sanchez

Mkunfunzi wa Manchester United Jose Mourinho amethibitisha kwamba klabu hiyo iko katika meza ya mazungumzo ya kumsajili shambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez
Image caption Mkunfunzi wa Manchester United Jose Mourinho amethibitisha kwamba klabu hiyo iko katika meza ya mazungumzo ya kumsajili shambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez

Mkunfunzi wa Manchester United Jose Mourinho amethibitisha kwamba klabu hiyo iko katika meza ya mazungumzo ya kumsajili shambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez na kwamba anasubiri habari njema.

MKufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji huyo wa Chile akajiunga na wapinzani wao katika ligi ya EPL.

Kiungo wa kati wa United Henrikh Mkhitaryan anatarajiwa kujumlishwa katika makubaliano hayo na kwamba hakuorodheshwa katika kikosi kitakachokabiliana na Burnley.

Hakuna haja ya kuficha ama kukataa lakini hatujaafikiana makubaliano.

Image caption Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez

Najua kwamba kila mtu anajua tuko katika meza ya mazungumzo na hususana baada ya mkufunzi wa Arsenal kuzungumza wazi.sanchez mwenye umri wa miaka 29 hayoko katika kandarasi na Arsenal mwezi Juni na andaiwa kuingia mkataba wa kibinafsi na klabu hiyo ya Old Trafford.

Mada zinazohusiana