Jimmy Armfield afariki Dunia.

Jimmy Armfied mtanganzaji mkongwe
Image caption Jimmy Armfied mtanganzaji mkongwe

Mtangazaji na mchezaji mkongwe wa Uingereza mwenye heshima kubwa, Jimmy Armfield amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 82 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani.

Pamoja na kuichezea mechi 569 Timu ya Blackpool enzi zake, pia alikuwa Nahodha wa England mara 15 katika mechi 43 alizochezea Simba Watatu.

Baada ya kuwa kocha wa timu za Leeds na Bolton, Armfield akahamia kwenye utangazaji na kujivunia heshima kubwa akiwa mchambuzi wa BBC Radio 5 Live. Na Familia yake imethibitisha kifo chake kilichotokea Trinity Hospice mapema asubuhi ya leo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii