Je, wewe ni mshambuliaji wa kimo cha futi sita inchi moja? Unaweza kupata kazi Chelsea

Andy Carroll, Christian Benteke, Peter Crouch, Ashley Barnes na Edin Dzeko Haki miliki ya picha PA, Getty
Image caption Andy Carroll, Christian Benteke, Peter Crouch, Ashley Barnes na Edin Dzeko

Mchezaji anayetafutwa ni lazima awe na urefu wa futi sita inchi moja, awe na uzoefu wa ligi ya EPL , umri na kasi yake sio muhimu lakini atahudumu kwa mkataba wa muda mfupi.

Chelsea bado hawajaweka tangazo hilo katika gazeti lolote magharibi mwa London mwezi Januari lakini kuna wakati ambapo utafutaji wa mshambuliaji ulionekana kuwa wa kukatisha tamaa.

Yamkini wanawatafuta wachezaji warefu wa kimo.

Andy Caroll, Ashley Barnes, Islam Slimani na Peter Crouch ni miongoni mwa wachezaji wanaohusishwa na uhamiaji wa kuelekea kwa mabingwa hao watetezi.

Mpango wao wa kumtafuta mshambuliaji huyo mrefu kwa kimo na ambaye atakuwa kwa mkopo ama kwa mkataba wa kudumu - umesababisha hali ya eti eti katika mitandao ya kijamii huku wachezaji nyota wa zamani wa mchezo huo wakitania kwa kutangaza kwamba wamejiondoa kutoka kwenye orodha ya wanaotafuta kazi Chelsea.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Gary Lineker aliandika kwamba ni mfupi mno kiasi kwamba hawezi pewa kazi Chelsea
Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Mshambuliaji wa Wycombe Adebayo Akinfenwa ni miongoni mwa waliotania hatua hiyo ya Chelsea

Mshambuliaji wa Roma na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Manchester City Edin Dzeko aliibuka kuwa mchezaji anayefaa ikilinganishwa na Lineker na Akinfenwa.

Lakini umri wake utafikia miaka 32 mwezi Machi, hawezi kushiriki katika Kombe la Klabu Bingwa Ulaya na bei yake ya £44m ikiwa katika mpango wa kubadilishana na beki wa kushoto Emerson Palmieri, ilifanya watu kuanza kuuliza lengo la uhamisho huo.

Miongoni mwa wale walioshangazwa ni wachezaji wa Chelsea wenyewe.

Eden Hazard ambaye amekuwa akicheza katika safu ya mashambulizi amesema kuwa Chelsea haihitaji mshambuliaji msimu huu, hususan 'mshambuliaji''.

Mchezaji huyo wa Ubelgiji alisema: Ni klabu gani bora msimu huu, Manchester City, washambuliaji wake sio warefu kwa kimo.

''Ni rahisi, iwapo unataka kucheza mpira wa pasi ndefu, unahitaji kulenga mtu na iwapo unataka mpira kuchezwa sakafuni, unahitaji watu wafupi.

Hivyo basi ni kwa nini mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte amejitahidi kuhakikisha kuwa anamsajili mchezaji wa ziada wa Alvaro Morata, na ni kwa nini kuna orodha kubwa ya majina?

BBC michezo inamuuliza mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Chris Sutton nani anafaa - na hatma ya klabu hiyo.

Ni wachezaji gani wanaolengwa na Chelsea?
Mchezaji Klabu Kimo Umri Mechi Mabao* Mashambulizi* Mashambulizi yaliolenga*
Ashley Barnes Burnley 6ft 1in 28 23 3 26 42.31
Christian Benteke Crystal Palace 6ft 3in 27 18 1 34 44.12
Andy Carroll West Ham 6ft 4in 29 12 2 18 38.89
Peter Crouch Stoke 6ft 7in 36 19 3 9 44.44
Edin Dzeko Roma 6ft 4in 31 20 9 90 36.70
Islam Slimani Leicester 6ft 2in 29 12 1 7 57.14
*Takwimu zote ni za msimu wa 2017-18

Dzeko amefunga mabao tisa katika ligi ya Serie A akiichezea Roma msimu huu lakini kati ya washambuliaji watano wa ligi ya Uingereza wanaohusishwa na Chelsea hakuna hata mmoja ambaye ameweza kufunga zaidi ya mabao matatu katika ligi hiyo. Christian Benteke ndio ,mchezaji wa pekee aliyechezeshwa zaidi ya mechi nane pia.

"Kwa kweli nimeshangazwa na idadi ya majina yaliotajwa , Sutton aliambia BBC michezo.

"Sijui habari ya Ashley Barnes ilitokea wapi lakini sidhani iwapo anaichezea Burnley mara kwa mara, Hivyobasi hilo litaisadia Chelsea kivipi? Kwa heshima kubwa hakuna vile atakavyowasaidia.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Barnes ameshiriki katika mechi 24 za Burnley msimu huu lakini 15 kati yake amecheza kama mchezaji wa ziada .Amefunga magoli matatu

"Kama shabiki wa Chelsea unatarajia kuwa wachezaji wanaosajiliwa wataleta mabadiliko katika timu lakini hilo sio wazo linalotiliwa maanani kwa sasa.

walitarajiwa kumnunua Alexis Sanchez wiki iliopita lakini sasa wako mbali kufanya ununuzi kama huo na watu wanaohusishwa nao.

Crouch na Caroll wamekuwa wazuri mbeleni lakini sasa ni wachezaji wa ziada katika vilabu vyao.

Je ni nani atakayesajiliwa kuwa mshambuliaji?

Conte anasisitiza hafanyi uamizi wa uhamisho wa wachezaji na hajasema chochote kuhusu wachezaji wanaolengwa ima athibitishe ama hata kukataa.

Lakini amezungumzia kuhusu mchezaji anayemtaka kama mbadala wa Morata ambaye hajafunga katika mechi sita ili kuongoza safu ya mashambulizi.

''Kwa maoni yangu ya soka , tunahitaji mshambuliaji ambaye tunaweza kumfananisha na mshambuliaji nyota wetu'' , Conte alisema baada ya timu yake kuishinda Brighton wikendi iliopita.

Anamaanisha kwamba mshambuliaji mbadala ambaye anaweza kudhibiti mpira na kuunganisha mchezo, na sio habari njema kwa mshambuliaji Michy Batshuayi.

''Nilidhani kuwa mchezo wa Mitchy Batshuayi ulikuwa mzuri siku ya Jumamosi'', alisema Sutton.

Lakini matamshi ya Conte yanatuambia kwamba hawezi kufanya kazi hiyo. Inaonekana kwamba ni mwisho wa barabara kwa upande wake.

Mchezo wa Chelsea uko wazi. Kama vile ambavyo Morata ni tishio kama alivyokuwa Diego Costa, ambaye mpango wake wa kurudi Atletico Madrid ulifanikiwa mwanzo wa mwezi Januari, hakuna hata mchezaji mmoja kati ya walioorodheshwa wanafanana na washambuliaji ambapo tayari wapo katika klabu hiyo.

''Crouch na Caroll sio washambuliaji wa kutegemea kwa kuwa sio tishio kwa mabeki kama vile Morata'' , alisema Sutton.

Hakuna hata mchezaji mmoja aliyeorodheshwa ambaye unaweza kumfananisha na mchezo wa Morata , swala ambalo linamfanya Eden Hazard ambaye amekuwa akitoa pasi nzuri kwa washambuliaji kupinga usajili huo.

Crouch, Caroll na Benteke hutegemea sana krosi huku mchezo wa Chelsea ukimtaka mshambuliaji kukimbia kimbia katika eneo hatari ili kuwakwepa mabeki.

Unapokuwa Hazard kila mara unapoenua kichwa unataka mshambuliaji unayeweza kumuona ambaye anajaribu kuwakwepa mabeki .

Kwa sasa Morata ametoa fursa hiyo. lakini nadhani Dzeko ndio mchezaji wa pekee anayeweza kutoa usaidizi zaidi kama huo miongoni mwa walioorodheshwa.

Morata anafaa kusahau fursa alizokosa kucheka na wavu ili kufanikiwa

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sutton alifunga bao moja la ligi ya Uingereza katika mechi 27 msimu wa 1999-00 kufautia uhamisho wake wa £10m kutoka Blackburn. Baada ya mwaka mmoja katika klabu hiyo ya The Blues alijiunga na Celtic kwa kitita cha £6m

Kushuka kwa kiwango cha mchezo wa Morata kunamaanisha kwamba kuna uvumi kuhusu hatma ya mchezaji huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 25 .

Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa dau la £60m lililovunja rekodi katika klabu ya Chelsea kutoka Real Madrid amekosolewa na baadhi ya mashabiki , vibaya kulingana na Sutton , ambaye anajua masaibu ya mchezaji anayelipwa pesa nyingi.

''Nadhani Morata anaweza kuwa mchezaji mzuri wa Chelsea'' , Sutton alisema.

Hawezi kuwa Coasta mwegine kwa sababu kuna Diego Costa mmoja , lakini Morata ana mchezo wake ulio tofauti.

Watu wamekuwa wakimkosoa kwa sababu amekosa nafasi nzuri lakini nadhani pia hana tamaa.

Nadhani Conte anafaa kumvumilia na mchezaji huyo ana uzoefu wa kutosha kuimarika tena.

Nilisoma mahojiano yake mwanzo wa msimu ambapo anakiri anaelekea nyumbani baada ya mechi na kufikiria kuhusu fursa alizokosa kufunga , lakini kwa yeye kufanikiwa ni lazima afute masaibu hayo katika akili yake.

Washambuliaji wote hupitia wakati mgumu kama yeye, ikiwemo washambuliaji bora kama Alan Shearer na Henrik Larson, lakini motisha yao haikushuka wakati hawakuwa wakifunga.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alvaro Morata alijiunga na Chelsea kwa kitita cha rekodi ya £60m kutoka Real Madrid mwisho wa msimu uliokwisha

"Nilikuwa na wakati ambapo nilikuwa nikijishuku , hususan wakati nilipokuwa Chelsea. Nadhani kitu kibaya ambacho naweza kufanya kama mshambuliaji ni kubabaika mbele ya lango, wakati mbegu ya kutojiamini inapojipanda akilini kama ilivyokuwa wakati wangu.

Nilikata tamaa na kukosa nafasi kadhaa. Nilikubali iniathiri wakati huo hata ijapokuwa nilijifanya jasiri na kufutilia mbali kwamba sikuwa katika hali yangu ya mchezo.

Katika kiwango hicho , wakati kichwa chako kinapokuwa na tashwishi kuhusu uwezo wako kama mchezaji ,unagundua na hilo ndilo linalomkera Morata.

Kwa sasa anaonekana kubabaika. Lakini alifunga mabao mazuri mapema msimu huu na sidhani amekuwa mchezaji mbaya ghafla-anafaa kujitafuta na kujipa nguvu ili kuweza kupita wakati huu mgumu

Kushuka kwa mchezo wa Alvaro Morata
Mechi 10 za kwanza Mechi 10 zilizoisha
Dakika alizocheza 722 800
Mabao 7 3
Dakika/mabao 103.1 266.7
Pasi za mabao 3 1
Mshambulizi 28 31
Mashambulizi 13 13
Mshambulizi yaliosababisha mabao 25 9.7

Je Conte atakuwa mkufunzi wa Chelsea kwa muda gani?

Conte amekuwa akikosolewa hivi karibuni na hatma yake baada ya msimu huu haijulikani.

Sutton anadhani hali ya mshambuliaji huyo itazidisha uvumi kwamba raia huyo wa Itali ataondoka Stamford Bridge hivi karibuni , licha ya kuwa na rekodi nzuri.

Umekuwa msimu mgumu lakini wamefanikiwa kufanya vyema katika ligi ya Uingereza hususan pointi walizopata, Sutton aliongezea.

Bado wako katika kinyang'anyiro na wana fursa ya kushinda mataji matatu -kombe la Carabao , lile la FA na kombe la vilabu bingwa hivyobasi Conte anaonekana kufanya vyema.

"Lakini kile kinachofanyika katika soko la uhamisho hakitawafurahisha mashabiki na kinakufanya kuuliza ni wapi klabu hii inaelekea .

Kwa kwli hivi sivyo Chelsea inavyofaa kujiendeleza , kupigania mataji ya ligi mbali na mataji makubwa na kukuwa kama timu.

Nadhani Chelsea itahusishwa na uhamisho wa wachezaji iliojaribu kuwasajili hapo awali , ambao Conte anawataka , kama vile Sanchez, Paulo Dybala na Gonzalo Higuain kutoka Juventus na sio watu wanaotoka kutamatisha soka yao katika klabu hiyo.

Mada zinazohusiana