Watanzania 9 kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika

Waamuzi tisa kusimamia mchezo wa shirikisho
Image caption Waamuzi tisa kusimamia mchezo wa shirikisho

Waamuzi nane kutoka Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika CAF kuchezesha mechi za ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Waamuzi wanne wameteuliwa kuchezesha mchezo wa Ligi ya mabingwa kati ya Lydia Ludic Burundi Academic ya Burundi na Rayon Sports ya Rwanda.

Mwamuzi Mfaume Ali Nassoro atakuwa mwamuzi wa kati akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Frank John Komba wakati mwamuzi msaidizi namba mbili atakuwa Soud Idd Lila na mwamuzi wa akiba Israel Omusingi Njunwa Mujuni huku kamishna wa mechi hiyo akitokea nchini Zimbabwe Gladmore Muzambi.

Mchezo huo utachezwa kati ya Februari 20 na 21, 2018 nchini Burundi.

Waamuzi wengine wanne wa Tanzania watachezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Masters Security Services FC ya Malawi dhidi ya Atletico Petroleos de Luanda ya Angola nutakaochezwa kati ya Febriari 20 na 21,2018 nchini Malawi.