Tetesi za Soka Alhamisi 25.01.18

Sergio Aguero Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sergio Aguero

Manchester City huenda ikaingia katika makubaliano na Atletico Madrid kubadilishana mshambuliaji raia wa Argentina Sergio Aguero, mwenye umri wa 29, ili kwa upande wake imchukue Antoine Griezmann, raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 katika msimu ujao wa joto. (Sun)

Lokomotiv Moscow imeifuata Liverpool kumtaka kumsajili winga mwenye umri wa miaka 23 Lazar Markovic. Msimu uliopita Mserbia huyo alichukuliwa kwa mkopo huko Sporting Lisbon na Hull City. (Mirror)

Chelsea imekubaliwa ombi lenye thamani ya pauni milioni 44, na marupurupu kwa msahmbuliajo wa Roma Edin Dzeko, na full beki raia wa Brazil Emerson Palmieri. (Guardian)

Kipa raia wa Uhispani wa Getafe Vicente Guaita, mwenye umri wa miaka 31, amefuzu ukaguzi wa kiafya huko Crystal Palace - lakini mazungumzo yangali yanaendelea kuhusu iwapo atajiunga na timu hiyo sasa au katika msimu wa joto. (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aden Flint

Brighton imewasilisha ombi la pauni milioni 6 kwa mlinzi wa Bristol City Aden Flint, aliyedhihirisha umahiri wake katika mashndano ya taji la Carabao. (Argus)

Klabu ya Ufaransa Monaco imekubali kumuuza mshambuliaji raia wa Argentina Guido Carrillo, kwa Southampton kwa pauni milioni 19.2. (Telegraph)

Sevilla imekubali makubaliano ya kumsajili mchezaji kiungo cha kati wa Swansea City Roque Mesa, mwenye umri wa miaka 28, kwa mkopo kwa muda uliosalia. (Marca - in Spanish)

West Ham inatarajiwa kumsajili raia wa Ureno Joao Mario, mwenye umri wa miaka 25, kutoka timu ya Inter Milan. Makubaliano ya awali yamefikiwa baina ya mchezaji huo na klabu hiyo ya Italia.

Meneja wa Barcelona Ernesto Valverde anasema klabu hiyo ya Uhispani haitosajili walinzi wengine wowote licha ya kuondoka kwa Javier Mascherano, 33, kuelekea katika ligi kuu ya Uchina timu ya Hebei Fortune. (ESPN)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Axel Tuanzebe

Aston Villa inakaribia kumaliza makubaliano ya kumchukua kwa mkopo beki wa kati wa timu ya Manchester United Axel Tuanzebe. (Express)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Sunderland Jack Rodwell,anafanyiwa majaribio katika timu ya Vitesse Arnhem. (Chronicle)

Mshambuliaji wa Ipswich Town David McGoldrick, mwenye umri wa miaka 30, anaonekana kulengwa tena na Cardiff City. (Wales Online)

Wachezaji wa West Brom James Morrison, na Chris Brunt, wameanza kuandaa taarifa ya pamoja kwa msimu ujao wa joto. (Express & Star)

Mchezaji mpya wa Manchester United Alexis Sanchez aikagua nyumba ya vyumba vitano vyenye thamani ya £2m - iliyo na chumba maalum kilicho na kinanda. (Mail)

Club America ya Mexico itamuekea vikwazo Carlos Darwin Quintero baada ya mchezaji huyo wa kiungo cha mbele mwenye umri wa miaka 30 kumpiga mpira mwandishi habari wakati wa matangazo ya moja kwa moja. (Goal)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii