Michuano ya FA Cup kuendelea kutimua vumbi tena hii leo

Image caption Kikombe la FA

Michuano ya FA Cup inaendele tena hii leo ijumaa kwa michezo miwili, Shifeld Wednesday wanawakaribisha Reading huku Manchester United wakiwa ni wageni wa Yovil katika dimba la Huish Park na Manchester kwa mara ya kwanza watamtumia mchezaji wao mpya waliye msajili kutoka kwa wapinzani wao Arsenal Alexis Sanchez.

Mara nyingi Manchester United inapokutana na Yovil imekuwa na matokeo mazuri zaidi, na kesho jumamosi Liverpool watakuwa wakicheza dhidi ya West Bromwich.

Wakati huo huo Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameongeza kandarasi ya kuendelea kukinoa kikosi hicho hadi mwaka 2020 , Mkataba wa kocha huyo ulitarajiwa kufikia mwisho mwaka 2019.

Mourinho amesema kuendelea kuwepo United kwa muda mwingine alioongezewa amesema yeye ni meneja sahihi kwa klabu kubwa kwa ajili ya malengo mengine na anamshukuru Mmiliki wa klabu hiyo Ed Woodward