Mourinho: Sanchez ameleta 'class' na ukomavu Manchester United

Mourinho amsifu Alexis Sanchez kufuatia ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Yeovil Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mourinho amsifu Alexis Sanchez kufuatia ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Yeovil

Uzoefu wa mchezaji Alexis Sanchez pamoja na ubora wake umeleta mwelekoo mpya katika safu ya mashambulizi ya klabu ya Manchester United, kulingana na mkufunzi Jose Mourinho.

Mchezaji huyo wa Chile , 29, alitoa pasi mbili zilizosababisha mabao mawili katika mechi yake ya kwanza katika klabu hiyo tangu uhamisho wake kutoka Arsenal katika ushindi wa 4-0 dhidi ya klabu ya Yeovil katika mechi ya raundi ya nne ya kombe la FA.

''Ni mchezaji mzuri sana'' , alisema Mourinho kwa BBC michezo.

''Uamuzi wake wa bao la pili ni chaguo ambalo mchezaji kama Marcus Rashford ni muoga kufanya''.

Aliongezea: Sancheza analeta klasi na ukomavu katika timu hii.

Sanchez alihamia Manchester United kutoka Arsenal siku ya Jumatatu huku mchezaji wa Man United Henrikh Mkhitaryan akielekea Arsenal.

Huku Zlatan Ibrahimovic akichezeshwa kama mchezaji wa ziada wa Romelu Lukaku katikati ya mashambulizi, Sanchez anatarajiwa kushindana na Rashford, Anthony Martial , Jesse Lingard na Juan Matta nyuma ya mshambuliaji.

Mada zinazohusiana