Wafukuza upepo mahiri kuchuana London

Ethiopia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kenenisa Bekele mwanariadha kutoka nchini Ethiopia

Mfukuza upepo maarufu kutoka nchini Ethiopia,Kenenisa Bekele anatarajiwa anatarajiwa kuchuana na raia wa Uingereza Mo Farah katika michuano ya Marthon ya mjini London mwezi wa nne mwaka huu.

Bekele ni mshindi mara tatu katika riadha kwenye michano ya Olimpiki na alikuwa wa pili nyuma ya mkimbiaji raia wa Kenya Daniel Wanjiru katika michuano ya mwaka wa jana.

Ninafurahi sana kurudi mjini London kwa mwaka wa tatu mfululizo na ningependa kuwa bora zaidi kuliko mwaka jana na kushinda katika michano hiyo, hiyo ni kauli ya Kenenisa Bekele.

Bekele anaongeza kusema kwamba ,Kwa mara ingine tena London imeleta wakimbiaji bora zaidi wa mbio ndefu duniani kwa pamoja na hivyo najua kuwa si rahisi."

Naye Eliud Kipchoge wa Kenya,ni bingwa wa marathon wa Olimpiki, ambaye alishinda michuano hiyo mwaka 2015 na 2016, pia atashiriki michuano hiyo ya London.

Bekele, Farah na Kipchoge wameshinda medali za dhahabu za Olimpiki zipatazo nane pamoja na medali za dhahabu 12 kati yao.

Mo amepewa cheo cha Sir, Eliud na Kenenisa wote wanapaswa konesha uwezo wa hali ya juu wenye ushawishi kwakuwa wao ni watajika katika tasnia ya riadha na sasa wanakutana kwa mara ya kwanza katika mbio za Marathon.