David Beckham amiliki timu

Uingereza Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David Beckham kiungo wa zamani wa timu ya Manchester United

Mchezaji wa zamani na kiongozi wa timu ya mpira wa miguu wa nchini Uingereza David Beckham amefanikiwa kuzindua mpango wake wa muda mrefu wa uzinduzi wa timu yake ya soka huko Miami.

Beckham alichungulia fursa hiyo katika harakati za kufunga mkataba timu yake ya zamani ya LA Galaxy mwaka 2014.

Timu hiyo haijatajwa mpaka sasa ingawa inatarajiwa kucheza mbele ya umati wa watu elfu ishirini na tano mjini Overtown na katika viwanja vilivyoko karibu na mji huo.

"ninafuraha kubwa kuileta timu hii kubwa kwenye jiji hili kubwa, ilikuwa ni safari ndefu na ngumu mpaka kufikia hapa nilipo leo anasema kiungo wa zamani wa timu ya Manchester United Beckham, mwenye umri wa miaka 42.Nina waahidi itakwenda katika ligi ikiwa ni timu bora anajinasibu David.

Baada ya uzinduzi huo David Bekham alipongezwa na watoto wake wanne kwa njia ya video maalum akiwemo mkewe Victoria, ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki wa zamani wa kundi la Spice Girl , mshindi mara 23 wa michuano ya Grand Slam Serena Williams, mshini mara nane wa medali ya dhahabu wa michuano ya Olimpic Usain Bolt na watu wengine maarufu akiwemo Brady, Will Smith, Jay Z na Jennifer Lopez.

Beckham, alijiunga na timua ya LA Galaxy akitokea timu ya Real Madrid mnamo mwaka 2007, na kuwa mchezaji wa kwanza mstaafu kumiliki timu katika ligi.

Image caption David Beckham na Wayne Rooney

Anajinasibu David kuwa alijiunga na timu ya Galaxy kwasababu alitambua uwezekano wa kudumu kwa muda mrefu katika ligi hii, "alisema.

Niliamua kuondoka Real Madrid na kwenda kwenye ligi ambayo ilikua inasuasua, ilikuwa ni hatua kubwa mno niliyopiga na kitu kimoja ninachokijua ni kuwa hatua hiyo itazaa matunda yenye changamoto lakini changamoto zenye kusisimua.

Kamishna Garber alikuja akaketi karibu yangu na kuanza kunieleza mipango ya ligi na wapi anapotaka kuifikisha nilikuwepo tangu siku ya kwanza.

Uzinduzi huu haikuwa kazi rahisi kwa muda wa miaka minne ya utafutaji kiwanja eneo la kusini mwa Florida huku tukipingwa na baadhi ya watu katika maeneo kadhaa.

Washirika wa David Beckham walinunua ardhi tayari kwa kujenga uwanja wao mnamo mwishoni mwa mwaka 2015, baada ya kushindwa mara tatu kununua eneo walilolitaka na bora zaidi kwa shughuli hiyo.

Serikali ya Miami ilifikishwa mahakamani na mfanyabiashara tajiri Bruce Matheson, aliyedai kuwa timu ya Beckham ilinunua ardhi haikununua kwa gharama stahiki na zabuni isiyokuwa na ushindani bila kufuata utaratibu. Madai hayo yalitupiliwa mbali, ingawa mfanya biashara huyo Matheson ameapa kukata rufaa.

Washirika wa Beckham ni pamoja na meneja wa zamani wa kundi la Spice Girls Simon Fuller, Mfanya biashara mwenye asili ya Bolivia na Marekani Marcelo Claure, Mfanya biashara kutoka Florida Kusini Jorge , Jose Mas na Mjasiriamali wa Kijapani JMasayoshi Son.