Tetesi za soka Ulaya Jumanne 30.01.2018

Chelsea itakataa ombi lolote kutoka Manchester City kumnunua nyota wake raia wa Ubelgiji Eden Hazard hata iwapo klabu hiyo ya Pep Guradiola inataka kuvunja rekodi ya £200m. (Telegraph)
Image caption Chelsea itakataa ombi lolote kutoka Manchester City kumnunua nyota wake raia wa Ubelgiji Eden Hazard hata iwapo klabu hiyo ya Pep Guradiola inataka kuvunja rekodi ya £200m. (Telegraph)

Chelsea itakataa ombi lolote kutoka Manchester City kumnunua nyota wake raia wa Ubelgiji Eden Hazard hata iwapo klabu hiyo ya Pep Guardiola inataka kuvunja rekodi ya £200m. (Telegraph)

The Blues inamlenga mshambuliaji wa Tottenham raia wa Uhispania Fernando Llorente, 32, iwapo watashindwa kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa na Arsenal 31 Olivier Giroud. (Sun)

Image caption Emre Can wa liverpool

Juventus wana matumaini wataweza kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na Ujerumani, 24, Emre Can ambaye kandarasi yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu, katika uhamisho huru (Mail)

Mkufunzi wa Everton Sam Allardyce amemwambia kiungo wa kati wa Uholanzi Davy Klaassen kwamba anafaa kwenda katika klabu nyengine kwa mkopo ili kuimarisha mchezo wake katika uwanja wa Goodison Park.

Image caption Davy Klassen

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alijiunga na Everton mwishoni mwa msimu uliopita hajachezeshwa hata mechi moja ya ligi ya Uingereza tangu mwezi Septemba.. (Star)

Kiungo wa kati wa Swansea Roque Mesa amepita ukaguzi wa kimatibabu katika klabu ya Sevilla.

Image caption Kiungo wa kati wa Swansea Roque Mesa amepita ukaguzi wa kimatibabu katika klabu ya Sevilla.

Mchezaji huyo wa Uhispania anatarajiwa kujiunga na timu hiyo ya La Liga kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Marca - in Spanish)

Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema kuwa klabu hiyo bado inamsaka kipa wa Getafe na Uhispania Vicente Guaita, 31, na beki wa Lille Ibrahim Amadou , 24 (Sky Sports)

Image caption Manchester City inakaribia kumsajili winga wa Uingereza wa kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Jack Harrison kutoka klabu ya New York City kwa dau la £4m.

Manchester City inakaribia kumsajili winga wa Uingereza wa kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Jack Harrison kutoka klabu ya New York City kwa dau la £4m.

Baadaye ataelekea katika klabu ya Middlesbrough kwa mkopo. (Mail)

Image caption Kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 25, amerudi katika klabu yake ya zamani kutoa kwaheri kwa wachezaji wenzake (Mail)

Kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 25, amerudi katika klabu yake ya zamani kutoa kwaheri kwa wachezaji wenzake (Mail)

Mkufunzi wa Burnley Sean Dyche amewasilisha ombi la kutaka kumsajili beki wa Nottingham Forest Joe Worrall, 21, kwa thamani ya £10m. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa kati wa zamani wa klabu ya Manchester United David Beckham ameshangazwa na hatua ya Arsenal kumuuza Alexis Sanchez, 29,

Kiungo wa kati wa zamani wa klabu ya Manchester United David Beckham ameshangazwa na hatua ya Arsenal kumuuza Alexis Sanchez, 29, na kusema kuwa ataleta ufanisi mkubwa katika klabu hiyo.. (Mirror)

Beckham pia inaamini kwamba Jose Mourinho ndio mtu anayefaa kuongoza Manchester United mbele. (Star)

Mada zinazohusiana