Siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho: Ni mchezaji gani atakayesajiliwa na Arsenal, Liverpool, Chelsea na West Ham?

Siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho inakamilika usiku wa saa sita.
Image caption Siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho inakamilika usiku wa saa sita.

Inaonekana kuwa siku itakayojawa na biashara nyingi za uhamisho wa wachezaji nchini Uingereza. Siku ya jumanne Manchester City ilimsaini beki wa Ufaransa Aymeric Laporte kwa dau lililovunja rekodi la £57m na hivyobasi kuongeza matumizi ya klabu za Uingereza kufikia £252m mwezi huu ikiwa ni rekodi katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.

Rekodi ya awali ilikuwa £225m ambayo iliwekwa 2011.

Beki wa Liverpool Virgil van Dijk aliyenunuliwa kutoka Southampton ndio uhamisho mkubwa nchini Uingereza mwezi huu. Lakini je ni nani atakayehama kabla ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho wa wachezaji siku ya Jumatano?

Manchester City

Klabu ya Manchester City tayari inapigiwa upatu kushinda ligi ya Uingereza na siku ya Jumanne walithibitisha usajili wa beki Laporte kutoka Athletic Bilbao.

Pia wanamtaka kiungo wa kati wa Shaktar Donetsk Fred, ijapokuwa inaonekana kwamba iwapo uhamisho huo utakamilika , raia huyo wa Brazil atasalia katika klabu ya Shakhtar hadi mwisho wa msimu.

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Kipa Ederson na beki wa kulia Kyle Walker wamefanya vyema tangu kujiunga kwao na manchester City katika dirisha la uhamisho wa mwisho wa msimu uliopita

Laporte ni mchezaji ambaye anapendwa na Guardiola, kwa kuwa mzuri sana anapokuwa na mpira.

Yeye hupeleka mpira hadi katikati ya uwanja na ni mchezaji mzuri wa City na City ni nzuri kwake.

City ilikuwa tayari kulipa Yuro 60m ili kumsajili 2016 lakini alisema kwamba hayuko tayari na alitaka kusalia katika klabu ya Bilbao.

Lakini miezi 18 baadaye wamemrudia na anasema kwamba yuko tayari. Anajua kwamba huu ndio wakati , kombe la dunia limesalia miezi sita kuanza na kwamba hajachezeshwa na Ufaransa.

Mkufunzi wa Ufaransa Didier Deschamps ana wasiwasi kumuhusu hususan kuhusu hali ya maungo yake .Hilo ndio swali kubwa juu yake wakati anapojiunga na ligi ya Uingereza.

Image caption Aymeric Laporte amesajiliwa na Manchester City

Manchester United haitarajiwi kutafuta mchezaji mwengine kufuatia kuwasili kwa Alexis Sanchez kutoka Arsenal .

Baadhi ya wachezaji akiwemo Matteo Darmian, Sergio Romero, Daley Blind na Maroune Fellaini wamehushishwa na uhamisho wa kuondoka katika klabu hiyo lakini mkufunzi Jose Mourinho anasema hakuna mchezaji atakayeondoka.

Zlatan Ibrahimovic anavutia klabu kama vile LA Galaxy lakini makubaliano hayo yanaweza kufanyika baada ya dirisha la uhamisho la Uingereza kukamilika

'Arsenal

Lengo kuu la Arsenal lilikuwa kumsajili mshambuliaji waBorussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang - lengo ambalo limetimia tayari.

Dortmund ilikuwa imesema kuwa itamuuza mchezaji huyo tu baada ya kupata mshambuliaji mwengine , na hadi kufikia sasa haijulikani iwapo mchezaji atakayechukua mahala pake ni mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba raia huyo wa Ufaransa ataondoka katika uwanja wa Emirates aidha kwa mkopo ama katika mkataba wa kudumu ili kuweza kupata fursa za kuchezeshwa mara kwa mara kabla ya kombe la dunia.

Image caption Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud

Itamshangaza kila mtu iwapo Arsenal itamruhusu Giroud kuelekea Chelsea, lakini iwapo Michy Batshuayi ataelekea Dortmund na Chelsea itashindwa kumsaini Edin Dzeko basi huenda Giroud akawekwa katika orodha ya wachezaji inaowataka.

Itaonekana makosa kumwacha Giroud kuelekea katika klabu pinzani.

Ni hali isiokuwa ya kawaida .Arsenal ingemsajili Aubameyang baada ya kukamilika kwa msimu uliopita huku Giroud akiwa mpango mbadala wake lakini walichelewa kwa muda mrefu wakijaribu kuchagua kati ya Abameyang na Alexandre Lacazette kabla ya kumchukua Lacazette kwa dau la £53m.

Na miezi sita baadaye wanaamua kwamba uamuzi waliofanya ulikuwa wa makosa na kulazimika kutumia £55m kumsajili Aubameyang, mshambuliaji ambaye mchezo wake unafanana kama ule wa Lacazette.

Image caption Pierre Emerick Aubameyang amejiunga na Arsenal kwa mkataba wa miaka mitatu

Iwapo Giroud anataka kwenda katika kombe la dunia , ni lazima achezeshwe na iwapo Arsenal ina Aubameyang na Lacazette basi italazimika kuondoka.

Chelsea

Chelseanayo huenda ikawa na biashara nyingi huku macho yote yakimlenga mshambuliaji.

Klabu hiyo imejaribu sana kumpatia mkufunzi Antonio Conte nguvu zaidi katika safu ya mashambulizi na msako wa kumtafuta mshambuliaji unamlenga Dzeko, 31 anayeichezea klabu ya Roma na mchezaji wa zamani wa Manchester City

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Edin Dzeko alifunga mabao 50 ya ligi ya Uingereza katika mechi 130 za Manchester City

Mkataba wa kumsajili mchezaji huyo wa Bosnian umecheleweshwa huku umri wake na fedha anazotaka kulipwa zikizua utata.

Kulikuwa na ripoti nchini Itali siku ya Jumatatu kwamba mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo ulikuwa umevunjika.

Je hatua hiyo itasababisha uhamisho wa Giroud, na je The Gunners watakubali kumuuza mchezaji wake kwa timu pinzani? na Je uamuzi huo unamaanisha nini kwa mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Batshuayi?

Image caption Batshuayi anazivutia timu za Sevilla na Borussia Dortmund

Batshuayi anatakiwa na Sevilla na Borussia Dortmund, huku kukiwa na mazungumzo na klabu hiyo ya Bundesliga kuhusu uhamisho wake.

Chelsea imefanikiwa katika harakati yake ya kusajili mchezaji mwengine wa Roma, beki Emerson Palmieri, ambaye anaelekea kujiunga na kikosi cha Conte kwa dau la hadi £23m.

Kuondoka kwa Philippe Coutinho na kuelekea Barcelona kumezunguka mjadala wa Liverpool kuhusu mpango wake wa uhamisho lakini kufikia sasa hakuna tangazo kubwa linalotarajiwa isipokuwa kuondoka kwa Danniel Sturridge aliyejiunga na West Brom..

Mkufunzi Jurgen Klopp hayuko tayari kujaza mapengo haraka haraka kama ilivyosubiri na kumnunua beki wa Southampton Van Dijik kwa dau la £75m baada ya kushindwa kumsajili mwisho wa msimu uliopita.

Image caption Nabu Keita kujiunga na Liverpool mwisho wa msimu huu

Huku kukiwa kuna hatari ya kutoweza kuimarisha kikosi , Liverpool iko tayari kusubiri hadi mwisho wa msimu huu ili kumsajili rasmi Naby Keita kwa dau la when they will sign Naby Keita for £51m -kwa lengo la kumpata mchezaji wanayemtaka.

Tottenham Hotspurs

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lucas Moura wa PSG

Kwa wiki tatu sasa inaonekana kana kwamba Tottenham haiko tayari kumsajili mchezaji yoyote kwa sasa licha ya kuhusishwa na usajili wa Lucas Moura.

Mchezaji huyo ambaye kwa sasa yuko mjini London amekuwa hachezeshwi na PSG. Akiwa na umri wa miaka 25 ,dau la £25m kwa mchezaji kama yeye ni fedha chache kwa Tottenham.

Ameonekana mara nyingine kwamba ana kipaji. Anahitaji mkufunzi ambaye anaweza kumsaidia kuimarika kitu ambacho Unai Emery na Laurent Blanc wameshindwa kufanya PSG.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danniel Sturidge alifunga katika kombe la dunia na michuano ya Yuro iliopita .Je ataelekea Urusi?

Mada zinazohusiana