Mesut Ozil asaini kandarasi mpya, Batshuayi aelekea Dortmund

Mesut Ozil Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mesut Ozil

Borussia Dortmund imekubali mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi kwa mkopo kwa kipindi cha msimu uliosalia, akisubiri kufanyiwa matibabu.

Arsenal ilimsajili mshambuliaji Pierre Emeric Aubameyang ambaye Dortmund wanasema watamuuza tu iwapo watapa mchezaji mwengine kuchukua mahala pake.

Chelsea huenda ikamsajili Olivier Giroud kutoka Arsenal ili kuchukua mahala pake Batshuayi ili kukamilisha mkataba wa miaka mitatu.

Wakati huohuo kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil ametia saini kandarasi ya miaka mitatu na nusu ili kusalia katika klabu hiyo hadi 2021.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mitchy Batshuayi

Ozil mwenye umri wa miaka 29 sasa ndio mchezaji anayepokea mshahara mkubwa katika klabu hiyo akijapatia kitita cha £350,000 kwa wiki kabla ya kulipa kodi.

Mkataba huo uliotiwa saini siku ya Jumatano, unajiri baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuhusu hatma ya raia huyo wa Ujerumani ambaye kandarasi yake ya awali ilikuwa inakaribia kuisha mwishoni mwa msimu huu.

Alijiunga na Gunners kutoka Real Madrid 2013 kwa rekodi ya uhamisho wa dau la £42.4m.

Mada zinazohusiana