Pierre-Emerick Aubameyang akamilisha kuhamia Arsenal kutoka Borussia Dortmund

Ni rasmi Pierre-Emerick #Aubameyang sasa ni mchezaji wa Arsenal, klabu hiyo ya London kaskazini imetangaza.
Image caption Ni rasmi Pierre-Emerick Aubameyang sasa ni mchezaji wa Arsenal, klabu hiyo ya London kaskazini imetangaza.

Ni rasmi Pierre-Emerick Aubameyang sasa ni mchezaji wa Arsenal, klabu hiyo ya London kaskazini imetangaza.

Aubameyang ametia saini mkataba wa "muda mrefu kwa uhamisho ambao umevunja rekodi ya klabu" kutoka Borrussia Dortmund.

"Mchezaji wetu wa pili wetu kumnunua wakati wa kipindi cha kuhama wachezaji Januari. Auba ni miongoni mwa washambuliaji stadi zaidi duniani. Amefunga mabao 98 katika mechi 144 akichezea klabu ya Dortmund ligi ya Bundesliga na amesaidia ufungaji wa mabao 172 katika mechi 213 ambazo ameshiriki akichezea klabu hiyo yake ya zamani michuano yote," Arsena wameandika kwenye mtandao wao.

Huwezi kusikiliza tena
Pierre-Emerick Aubameyang

The Gunners waliwasilisha maombi mawili ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ambayo yalikataliwa na Dortmund kabla ya kukubali dau la juu ya £46.5m walilomsajilia Alexandre Lacazette.

Image caption Mkufunzi wa Arsenal Arseene Wenger

Dortmund ilikuwa imesema kuwa itamuuza mcheza huyo baada ya kupata mbadala wake huku mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi akitarajiwa kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo.

Aubameyang alifunga mabao 141 katika mechi 213 akiichezea Dortmund tangu 2013, ikiwemo mechi 21 kati ya 24 msimu huu.

Lakini alipigwa marufuku na klabu hiyo ya Ujerumani katika mechi yao dhidi ya Wolfsburg tarehe 14 Januari kwa kukosa mkutano wa timu.

Mshambuliaji huyo pia aliwachwa nje kwa mechi yao dhidi ya Hertha Berlin kwa sababu maafisa wa klabu hiyo walihisi hakuwa na malengo lakini alicheza dakika 90 katika mechi ya Jumapili dhidi ya Freiburg.

Ameichezea Gabon mara 56 akifunga magoli 23.