Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 02.02.2018

Riyad Mahrez Haki miliki ya picha Getty Images

Winga wa Leicester na Algeria Riyad Mahrez, 26, huenda akapigwa faini ya £200,000 na klabu hiyo iwapo ataendelea kususia mazoezi baada yake kuzuiwa kuhamia Manchester City. (Mirror)

West Ham walishindwa kumnunua mshambuliaji kutoka Algeria Islam Slimani, 29, kwa sababu Leicester walikataa kufanya biashara na Karren Brady baada ya mwenyekiti huyo wa West Ham kunukuliwa gazetini akizungumzia kufutwa kwa meneja wa zamani wa Leicester Claudio Ranieri. Slimani amehamia Newcastle kwa mkopo. (Guardian)

Manchester United wataangazia kumtafuta kiungo wa kati ambaye atamsaidia Mfaransa Paul Pogba, 24 kufikia upeo wake wa uchezaji soko litakapofunguliwa mwisho wa msimu. (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images

Arsenal watajaribu tena kumtafuta fowadi Mbrazil Malcom, 20, kutoka Bordeaux majira ya joto, na huenda wakamtafuta pia kipa wa Atletico Madrid kutoka Slovenia Jan Oblak, 25, kutafuta mlinda lango wa kuchukua nafasi ya Petr Cech, 35. (Evening Standard)

Wachezaji wenzake Mahrez wameghadhabishwa na hatua yake ya kukosa kuhudhuria mazoezi, lakini naye anahisi kwamba alisalitiwa na klabu hiyo. (Sun)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte ataondoka klabu hiyo mwisho wa msimu. (Guardian)

Conte, 48, anatarajiwa kupewa nafasi ya kuondoka Stamford Bridge kwa kupewa kazi ya kuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Italia tena. (Sun)

Lakini Blues wanatumai kwamba anaweza kuangazia kandanda pekee, hasa sasa baada ya dirisha la kuhama wachezaji kufungwa. (Telegraph)

Manchester United wanataka meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino achukue nafasi ya Jose Mourinho atakapoondoka Old Trafford. (Manchester Evening News)

Viongozi wa Serie A Napoli walikuwa tayari wameanza kupoteza hamu ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi anayechezea Everton Davy Klaassen, 24, kabla ya mzozo kuhusu haki za picha zake kutibua mpango wake wa kuhama siku ya mwisho. (Liverpool Echo)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ademola Lookman

Kiungo wa kati wa Schalke Mjerumani Max Meyer ataamua kuhusu mustakabali wake wiki chache zijazo, huku Arsenal na Barcelona wakidaiwa pia kumnyatia mchezaji huyo wa miaka 22. (Star)

West Brom wanaandaa mazungumzo kuhusu mkataba wa beki wao Jonny Evans, 30, baada yao kufanikiwa kumzuia kuhama Januari. Evans ana kifungu cha £3m cha kumfungua kutoka kwa mkataba wake iwapo klabu hiyo itashushwa daraja. (Daily Mail)

Tottenham wanapanga kumtafuta beki wa kushoto wa England anayechezea Fulham Ryan Sessegnon, 17, majira ya joto na wanataka kutafuta mchezaji atakayekaa nao kwa muda mrefu kujaza pengo la kiungo wa kati kutoka Ubelgiji Mousa Dembele, 30. Mchezaji wa Norwich kutoka England James Maddison, 21, ni mmoja wa wanaolengwa na kalbu hiyo. (Evening Standard)

Inter Milan sasa wana nafasi nzuri ya kumnunua mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 20, kutoka Racing Club, baada yake kuanza pia kutafutwa na mahasimu wa ligi Uhispania Atletico Madrid na Real Madrid. (AS - kwa Kihispania)

Real Madrid wanamnyatia kipa wa Roma wa miaka 25 kutoka Brazil Alisson, ambaye anatafutwa pia na Liverpool. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Mkurugenzi wa michezo wa Roma, Monchi anasisitiza kwamba hakuna klabu iliyowasilisha ofa kumtaka Alisson Januari. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Davy Klaassen alikuwa nahodha wa Ajax fainali ya Europa League msimu uliopita walipolazwa na Manchester United

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Leander Dendoncker anafanya mazungumzo kumfungua kutoka kwa mkataba wake na Anderlecht baada ya klabu hiyo kukataa ahamie West Ham siku ya mwisho ya kuhama kwa wachezaji Januari. (Het Laatste Nieuws - kwa Kiholanzi)

Crystal Palace pia waliwasilisha ofa kumtaka Dendoncker, 22, lakini walichelewa na hawakufanikiwa kukamilisha mkataba, kwa mujibu wa meneja wa Anderlecht Herman van Holsbeeck. (Sporza - kwa Kiholanzi)

Everton walitaka winga wao Ademola Lookman, 20, kwenda Derby kwa mkopo, lakini raia huyo wa England alilamimisha uhamisho wa kwenda RB Leipzig kwa mkopo. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati wa Sunderland, Mwingereza Jack Rodwell, 26, alikataa nafasi ya kuhamia klabu nyingine Januari, licha yake kuomba aruhusiwe kuondoka na Sunderland kujitolea kuvunja mkataba wake wa kulipwa £70,000 kwa wiki. (Chronicle)

Celtic walikataa juhudi za dakika za mwisho kutoka kwa Crystal Palace siku ya mwisho ya kuhama wachezaji kumtaka mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele, 21. (Scottish Sun)

Meneja wa Lille Christophe Galtier atazungumza na Ibrahim Amadou baada ya beki huyo wa miaka 24 kutoka Ufaransa kukosa kuhudhuria mazoezi. Nahodha huyo wao alisafiri London siku ya mwisho ya kuhama wachezaji lakini akashindwa kujiunga na Crystal Palace. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sunderland wameshinda mechi moja pekee Jack Rodwell akiwa kikosi cha kuanza mechi misimu mitatu iliyopita

Real Sociedad wameahidi kubadilisha fulana za mashabiki zilizo na jina Inigo Martinez bila malipo, baada ya beki huyo Mhispania kujiunga na mahasimu wao Athletic Bilbao kwa euro 32 milioni (£28m). (El Pais - kwa Kihispania)

Meneja wa Borussia Dortmund Peter Stoger amekiri kwamba ana furaha kwamba mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 28, aliondoka klabu hiyo na kujiunga na Arsenal siku ya mwisho ya kuhama wachezaji. (Bild - kwa Kijerumani)