Olimpiki: Sabrina Simader ni Mkenya anayetafuta dhahabu kwenye 'barafu'.

Sabrina Simader wa Kenya Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sabrina Simader ni Mkenya wa kwanza anayeitafutia Kenya dhahabu katika mchezo wa kuteleza barafuni kwa kutumia ubao, michezo ya Olimpiki ya majira ya joto

Wakati Sabrina Simader alipoelekea Austria kutoka Kenya alifurahishwa na barafu

Miaka kadhaa baadaye , mapenzi yake ya kuteleza milimani kwa kutumia ubao nchini Austria yalibadilika na kuwa hamu kubwa ambayo imemweka katika barabara ya kuandikisha historia, ambapo msichana huyo mweye umri wa miaka 19 anatarajiwa kuwa mwanamke wa kwanza atakayeiwakilisha Kenya katika mchezo wa kuteleza barafuni kwa kutumia ubao katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi.

Ilikuwa ndoto ya babangu wa kambo kuiwakilisha Kenya katika michezo ya Olimpiki , Simader aliambia BBC kabla ya kuongeza: na Ndoto yangu pia.

'Msichana huyu ana ustadi wa kuteleza barafuni'

Safari yake katika michezo ya Olimpiki mjini Pyeongchang 2018 , Korea Kusini ilianza wakati alipokuwa na miaka mitatu pekee.

Babake wa kambo Josef alikuwa akimiliki ubao wa kutelezea na alipendelea kumpeleka Simadar katika milima.

Alimfunza kuteleza na kumuelezea kile alichohitaji kujua Lakini akiwa mtelezaji wa pekee mweusi katika eneo hilo, uwepo wake katika barafu ulikuwa ukiwavutia wengi.

''Shuleni nilikuwa msichana mweusi wa pekee'' , alisema. ''Mara ya kwanza ilikuwa vigumu kwa kuwa kila mtu alikuwa akiniangalia''.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Simader ni mzaliwa wa Kenya , lakini akaelekea Austria wakati alipokuwa na miaka mitatu.

Lakini alipoendelea kufanya vyema katika mchezo huo , anasema kwamba watu walianza kuvutiwa na mbinu zake na kasi.

"Walishangaa kwamba msichana mweusi ana uwezo wa kuteleza hivyo'', alisema.

Mara ikabainika wazi kwamba ndoto yake waliokuwa nayo na babake huenda ikafanikiwa, na licha ya kukuwa nchini Austria na kuhudumu maisha yake yote, Simader anasema kwamba kwa kuchagua kuiwakilisha Kenya halikuwa wazo gumu.

''Mamangu ni Mkenya, familia yangu inatoka Kenya'', alielezea. Sitaki kuiwacha nchi yangu

Mara ya mwisho yeye kuzuru Kenya ilikuwa miaka mitano iliopita , lakini Simader anasema kuwa ameungwa mkono na kupata usaidizi mwingi kutoka kwa raia wa Kenya .

''Wakenya wamefurahishwa sana'' , alisema. ''Wamekuwa wakinisaidia sana na hilo linanipatia nguvu zaidi''.

Simader alifuzu katika michezo hiyo baada ya kushiriki katika mashindano ya dunia Februari iliopita , na hivyobasi kuwa Mkenya wa pili baada ya Phillip Boit kuliwakilisha taifa hilo la Afrika mashahriki katika michezo hiyo ya majira ya baridi.

Pia aliiwakilisha Kenya katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi miongoni mwa vijana nchini Norway, wakati alipoorodheshwa miongoni mwa wachezaji 25 bora katika mashindano yote aliyoshiriki.

Lakini licha ya usaidizi mwingi kutoka kwa Wakenya , Simader anasema kuwa mambo yamekuwa 'magumu' upande wa kamati ya kitaifa inayosimamia michezo ya Olimpiki, kitu ambacho anasema kinatokana na ukosefu wa ufahamu kuhusu mchezo huo , vifaa na gharama zake nyingi.

BBC imewasiliana na kamati hiyo na inasubiri majibu.

Simader anakadiria kwamba itagharimu $250,000 kufadhili msimu mzima na ijapokuwa NOC ilimsaidi wakati wa michezo ya dunia mnamo mwezi Februari, amepata usaidizi mkubwa kutoka kwa wafadhili wake wanne, ambao anasema bila wao asingeweza kupata ufanisi alionao kwa sasa.

Ili kutimiza ndoto yake sasa ameomba usaidizi kutoka kwa Wakenya.

Na huku akijiandaa kwa mashindano hayo , Simader anasema kuwa watu wengi wameanza kumtazama tena.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sabrina Simader wa Kenya wakati wa mashindano ya dunia ya kuteleleza barafuni kwa kutumia ubao

Ni mwanamke wa Afrika wa pekee ambaye amefuzu mashindano ya kuteleza barafuni katika michezo hiyo na nje ya Austria bado hajulikani. lakini macho ya watazamaji hao hayamgutushi.

Lengo lake katika michezo hiyo ni rahisi, kushindana vyema na kuuonyesha ulimwengu kwamba Msichana wa Kenya anaweza kuteleza barafuni kwa kasi zaidi.