Aubameyang augua baada ya kuwasili Arsenal, je atacheza wikendi?

Aubameyang augua homa baada ya kuwasili Arsenal Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aubameyang augua homa baada ya kuwasili Arsenal

Pierre-Emerick Aubameyang anaugua lakini huenda akaanzishwa kwa mara ya kwanza na Arsenal katika mechi dhidi ya Everton itakayochezwa katika uwanja wa Emirates.

Arsenal ilivunja rekodi yao ya uhamisho baada ya kumleta mchezaji huyo kutoka Borussia Dortmund kwa dau la £ 56m katika siku ya mwisho ya uhamisho.

Na Arsene Wenger amesema huenda mchezaji huyo akaongoza safu ya mashambulizi kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu.

Wenger amesema kuwa Auba atakaguliwa kimatibabu kabla ya mechi ya Arsenal dhidi ya Everton hapo kesho.

''Lazima akaguliwe maungo , alikuwa na homa kwa hivyo hakuweza kufanya mazoezi mengi. Alianza jana, lakini bado hajapona . Nitafanya ukaguzi na idara ya matibabu nione iwapo atakuwa tayari kwa siku ya Jumamosi'', alisema Wenger katika mkutano wake na vyombo vya habari.

''Wenger pia aliwaelezea waandishi lengo lake la kumsajili Auba. Ni mshambuliaji mwenye kasi na uwezo wa kufunga mabao katika mechi anazocheza'', alisema Wenger.

Wakati huohuo raia huyo wa Ufaransa pia alifichua kwamba mchezaji wa zamani wa Arsenal amekuwa akifanya mazoezi katika klabu hiyo ili kuimarisha maungo yake huku akitafuta klabu mpya baada ya kuachiliwa na klabu ya Urusi Rubin kazan.

''Anatafuta klabu mpya, hakuna zaidi, akifutilia mbali uwezekano kwamba huenda akaichezea tena Arsenal''.

Mada zinazohusiana